Baada ya mkali wa single mpya ya 'Ntampata wapi' Diamond Platnumz kutua nyumbani Tanzania katika jiji la Dar es
salaam December 2 akitokea Afrika Kusini baada ya kunyakua tuzo tatu za Chanel O Music Video Awards 2014 ambapo alipata nafasi ya kukutana na wadau,
mashabiki pamoja na waandishi wa habari pale Escape 1
kuzungumzia ushindi wake na uwakilishi wake kama Mtanzania na Mwana Afrika Mashariki katika tuzo hizo.
Katika kuzungumzia vitu muhimu kiongozi huyo wa kundi la Wasafi Classic Baby 'WCB' alieleza mambo ambayo hukwamisha mafanikio ya wasanii wengi wa Tanzania ikiwemo swala zima la Ushirikiano baina yao na pia maswala ya beef zisizo na maana zaidi ya kuleta makundi na maelewano hasi kwa mashabiki wao na huku akizidi kusisitiza kuwa miongoni mwa vitu muhimu ni umoja unaohitajika kwa wasanii wa Tanzania ili
waweze kuwa wengi katika majukwaa ya kimataifa.
“Ombi langu mimi kiukweli ni moja tu, Unajua lazima
kama alivyosema mheshimiwa hapa muziki wetu
ushakuwa, watu wanaukubali na tushaona njia
kama tunaweza so lazima sisi tujiamini wenyewe
tusikaekae sana nyuma kwasababu watu kuna ile
kuogopa cha kuona kama aah! watanipokea kweli.
Na zile za aah! ntashindwa kuongea kizungu
ntachekwa mi nishachekwa sana kwenye kizungu
sana, lakini saizi naweza nikaingia hata Big Brother
na broken zangu hivyo hivyo lakini napita hivyo
hivyo nimeingia pale juzi Fally hajaongea mi
nimeongea “. alisema Diamond.
Platnumz pia aliendelea kuwaomba wasanii
wenzake kutotengenezeana beef za wenyewe kwa
wenyewe “Kingine mimi nilikuwa nataka niombe tufute zile
zama zakutengenezeana matatizo wasanii
wenyewe kwa wenyewe wa Tanzania kwasababu
haiwezi kutusaidia kabisa".
VIPI KUHUSU ALLY KIBA?.
Katika jambo ambalo nililiona la maana na la msingi wakati Diamond akiongea hayo ni baada ya kuongea maneno yaliyo onyesha dhahiri kuwa beef lake na Ally Kiba limekwisha na alicho sema ni hiki:
"nilivyofika Nigeria nilikuwa najiona
kama mkiwa kwasababu niko peke yangu,
nikiangalia huku simuoni hata Jaguar, huku siwaoni
wasanii wenzangu namtafuta Dimpoz namtafuta
nani, hata Ally simuoni yaani niko peke yangu.”
SHARE + COMMENT.
No comments: