Recent Posts

SPORTS: ARSENAL KURUDIA HISTORIA YA MWAKA 2005 MBELE YA MAN U?.

ARSENAL KURUDIA HISTORIA YA MWAKA 2005
MBELE YA MAN U?.

>>Wababe wa ligi kuu England Manchester United na Arsenal leo wanavaana katika uwanja wa Old
Trafford katika mchezo wa robo fainali za mashindano ya FA Cup huku mashabiki wa soka wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi
walioupata vijana wa mzee Wenger mwaka 2005, kutoka mikononi mwa wapinzani wao hao wakubwa wajulikanao kama Mashetani wekundu.

Katika mpambano huo wa fainali uliofanyika katika dimba la Millenium Studiuma, Arsenal waliibuka washindi kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 za kipute hicho bila kufungana.

Timu zote mbili zimekwishabeba kombe hilo mara 11, Ni kweli FA Cup si lolote? Bosi wa Manchester
Utd Louis van Gaal amesema kuwa kumaliza ligi huku ukiwa katika nne bora ni jambo la muhimu sana kwake yeye kuliko hata kuishinda kombe la FA.

Kauli ya kocha huyo inakuja huku kukiwa imebaki saa kadhaa kwa Manchester Utd kuvaana na
wapinzani wao wa muda mrefu Arsenal. ‘’Kumaliza katika nafasi nne za mwanzo ni matokeo bora na
kwa sisi Manchester Utd nafikir ni bora zaidi’’ alisema Van Gaal.

'’Kama unashinda kombe la FA
huingii katika mashindano ya klabu bingwa lakini ndo umekuwa bingwa’’ aliongeza.

Manchester Utd inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ya England kwakuwa na point 53
ikitofautiana point moja tu na wapinzani wao Arsenal iliyo nafasi ya tatu wakiwa na point 54, huku nafasi ya tano ikishikwa na Liverpool yenye point 51.

SPORTS: ARSENAL KURUDIA HISTORIA YA MWAKA 2005 MBELE YA MAN U?. SPORTS: ARSENAL KURUDIA HISTORIA YA MWAKA 2005
MBELE YA MAN U?. Reviewed by Unknown on 08:03 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.