UMESIKIA HII KUHUSU MTANGAZAJI WA BBC
(CHARLES HILLARY).
Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania
Charles Hillary aliyewahi kusikika sana kupitia Radio One.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka ndani ya Shirika hilo limesema Hillary sasa anarudi nyumbani anakwenda kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam.
Kwa mujibu wa Mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaarifu wafanyakazi
wake juu ya kuondoka kwa Hillary na kusema amefanya kazi ya Utangazazji kuanzia mwaka 1994
alipojiunga na Radio one na kabla ya hapo alitokea radio Deutsch Welle na baadaye mwaka 2006
alijiunga na BBC.
Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alisema Hillary anatarajia kujiunga na kituo hicho na kuelezea furaha yake ya kufanya kazi tena na
mtangazaji huyo mchangamfu.
No comments: