Klabu ya
Arsenal imeshindwa kuongoza ligi kuu nchini England baada ya kufungwa mabao 4-0
na Southampton katika mchezo uliopigwa jana usiku katika dimba la St Mary.
Mabao kutoka
kwa Cuco Martina, Shane Long (2) na Jose Fonte yaliisaidia Southampton kupata
point tatu muhimu mbele ya The Gurnners ambao awali walitarajiwa wangeshinda
mchezo huo.
Mchezaji wa Southamptoni Shane Long
aliyefunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Arsenal.
|
Kwa upande wa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alishindwa kuendeleza ubabe wake baada ya wiki iliyopita kuifunga anchester City siku ya Jumatatu, lakini walipofika kwa Southampton hawakufua dafu na kukubali kipigo hicho cha mabao 4-0.
Matokeo yote
Mechi za jana.
Sat 26 Dec 2015 - Premier League
- Stoke 2 - 0 Man Utd
- Aston Villa 1 - 1 West Ham
- Bournemouth 0 - 0 Crystal Palace
- Chelsea 2 - 2 Watford
- Liverpool 1 - 0 Leicester
- Man City 4 - 1 Sunderland
- Swansea 1 - 0 West Brom
- Tottenham 3 - 0 Norwich
- Newcastle 0 - 1 Everton
- Southampton 4 - 0 Arsenal
ARSENAL YAPIGWA 4-0 NA SOUTHAMPTON
Reviewed by Unknown
on
22:28
Rating:
No comments: