>>Mchezaji kutoka Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani ya bara la Afrika.
Samatta ametwaa tuzo hiyo kutokana na mafanikio yake katika Klabu ya TP Mazembe ambapo aliiwezesha kutwaa taji la klabu bongwa Africa huku yeye akiwa mfungaji bora wa mashindano hayo.
Kwa upande wa mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon na klabu ya Borussia
Dotmund ya nchini Ujerumani Pierre-Emerick Aubemeyang ametwaa tuzo ya
mchezaji bora wa bara la Afrika huku akiwashinda Yaya Toure na Andrew
Ayew.
Kocha bora wa mwaka ni Herve Renard kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo.
Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon wakati tuzo ya mwamuzi bora wa mwaka imeenda kwa Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.
Timu ya taifa ya Ivory Coast imekuwa timu bora ya mwaka na kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya taifa ya Cameroon ya wanawake.
Klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

MBWANA SAMATTA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA
Reviewed by Unknown
on
03:35
Rating:

No comments: