Recent Posts

CHRIS BROWN MIKONONI MWA POLISI TENA BAADA YA KUMPIGA KOFI MWANAMKE WA WATU!.


MWAKA 2016 ukiwa ndo unafunguka nyota na mkali wa nyimbo za RnB Chrisbrown ambaye kwa sasa yupo kimauzo zaidi katika muziki na Albamu yake ya ‪#‎Royality‬ amaingia katika matatizo baada ya kumzaba kofi Mwanamke moja aliye julikana kwa jina la Liziane Gutierrez katika club ya ‪#‎The_Palms_Casino_Resort‬, LAS VEGAS Marekani jumamosi ya wiki iliyopita ikiwa ndo ya kwanza kwa mwaka 2016.

Mkasa huo unadaiwa kutokea wakati Chris Brown akiwa katika Club hiyo kama nafasi ya kusheherekea siku ya pili ya mwaka ambapo Mwanamke huyo alijaribu kumpiga picha pasipo idhini yake ndipo ikadaiwa Chris Breezy alimpiga kofi la uso na kuharibu furaha ya Mwanamke huyo na hivyo kwenda moja kwa moja kumlipoti Polisi kwa kitendo alicho fanyiwa!.

Polisi mjini Las Vegas wakiwa bado katika uchunguzi wa Tuhuma hizo tukio hili likiwa linafungua mwaka lime urudisha nyuma (TBT) ulimwengu kwa kuweka mrejesho wa tukio kama hili la mwaka 2009 ambapo Breezy alimpiga na kumuumiza aliye kuwa mpenzi wake Robin Fenty "RIHANNA".

TEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK NA LIKE KWA TAARIFA MBALI MBALI.
m.facebook.com/KAYSTALLION.TZ

CHRIS BROWN MIKONONI MWA POLISI TENA BAADA YA KUMPIGA KOFI MWANAMKE WA WATU!. CHRIS BROWN MIKONONI MWA POLISI TENA BAADA YA KUMPIGA KOFI MWANAMKE WA WATU!. Reviewed by Unknown on 04:12 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.