Kwa upande wa Rais wa Marekani Barack Obama amekuwa mtu muwazi sana akimkubali mtu hasa kwa upande wa wasanii kama ilivyo kuwa kwa akina Snoop Dogg, Pharel Williams na mastaa wengine walio wahi kuitwa na Rais Obama kwenda kuonana naye na kupokea pongezi kwa kazi zao nzuri ndivyo ilivyo kuwa pia kwa mkali wa hit song "King Kunta" Kendrick Lamar.
Sababu za Kendrick Lamar kuitwa Ikulu kwa Obama "WHITE HOUSE" ni pamoja na kwamba Kendrick ni miongoni mwa mastaa wa Rap Music anao wakubali sana na alisha wahi kudiliki kusema kuwa katika Play List yake ya Muziki anayo isikiliza kwa siku nyimbo ya Kendrick "How Much A Dollar Cost" Ilikuwa inahusika pia.
Kendrick Lamar kama msanii mkubwa ambaye pia ameisha wahi kuwa Nominated kwenye tuzo 11 za Gramy Awards pamoja na Album Bora ya mwaka 2015 "To Pimp A Butterfly"
aliitwa Ikulu kwa Obama ikiwa ni sehemu ya pongezi kwa kazi zake nzuri lakini kubwa zaidi ni kuhusu video yake ya "Pay It Forward" ambayo ipo kiharakati ikielezea suala zima la kiushauri wa Maisha hasa kwa vijana na Video hii kimtazamo inataka kuendana na video clip ya Kendrick ya "Hard Work" kwa kuelezea juu ya video hiyo ya PAY IT FORWARD, Kendrick alisema kuwa alipo kuwa mdogo alikuwa hapendi kushauriwa lakini kilikuja kuwa kitu kilicho mgharimu kwa baadhi ya maeneo ya Maisha yake.
"Binafsi nilipo kuwa bwana Mdogo nilikuwa sipendi Mashauri lakini kutokana na hali ya maisha ilivyi niliweza kujifunza katika hilo na kugundua ina gharimu hivyo nikajirekebisha na natumia fursa ya hii video ya "Pay It Forward" kama sehemu ya kumuelimisha na kumuelekeza kijana mdogo kama mimi nilivyo kuwa kwa habari ya Maisha", alisema Kendrick.
FAHAMU: Hii inakuwa mara ya Pili Kendrick kukutana na kujadili mambo na Rais Obama hasa ya Kijamii baada pia ya kuwahi kukutana mwezi Octoba mwaka jana mjini Washington, D.C. wakati akipafomu katika tamasha kwenye ukumbi wa Kennedy Center ambapo waliweza kujadili maswala ya kijamii kwa miji na maeneo ya Marekani ikiwa pia na kujadili matatizo na namna ya kuyatatu kupitia mfumo wa sanaa ya uimbaji hasa anayo ifanya Kendrick.
UNAWEZA KUTEMBELEA UKURASA WETU WA FACEBOOK NA KU LIKE ILI USIPITWE NA HABARI MBALI MBALI TEMBELEA HAPA ......(OUR FACEBOOK PAGE)
KENDRICK LAMAR AITWA NA OBAMA IKULU NA HII NDIYO SABABU!
Reviewed by Unknown
on
04:44
Rating:
No comments: