Recent Posts

MAN UTD WASIMAMISHWA NA NEWCASTLE

Georginio Wijnaldum alifungia Newcastle bao la kwanza
Klabu ya Manchester Utd imeshindwa kupata ushindi baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3  na Newcastle United katika mchezo wa ligi kuu nchini England uliopigwa katika dimba la  St James Park.

Mashetani wekundu Man utd ndio walianza kupata bao kupitia kwa nahodha wake Wayne Rooney  kwa mkwaju wa penalti kisha kinda Jesse lingard akaongeza bao la pili katika dakika ya 3.

Katika dakika ya 42 kiungo Georginio Wijnaldum akaifungia Newcastle bao la kwanza na mshambuliaji Aleksandar Mitrovic akasawazisha bao la pili kwa upande wa timu yake kwa mkwaju wa penalti.

Rooney kwa mara nyingine aliweka Man Utd mbele kwa kuongeza bao la tatu. Lakini ikiwa imesalia dakika moja mpira kumaliza beki Paul Dummett alitikisa wavu na kufanyas mchezo kumalizika sare ya mabao 3-3.

Kwa upande wa Wagonga nyundo wa London West Ham katika mechi nyingine wamechomoza na ushindi wa mabo 3-1 dhidi ya Bournemouth, Enner Valencia akifunga mabao mawili na Dimitri Payet akitupia moja huku bao la Bournemouth likifungwa na Harry Arter.

Nao Aston Villa wamepata ushindi wao wa kwanza chini ya meneja Remi Garde kwa kuichapa Crystal Palace bao 1-0, bao lilofungwa na Joleon Lescott. Hata hivyo Villa wanaendela kuburuza mkia wakia na alama 11.
MAN UTD WASIMAMISHWA NA NEWCASTLE MAN UTD WASIMAMISHWA NA NEWCASTLE Reviewed by Unknown on 02:27 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.