Klabu ya Liverpool imekamilisha usajiri wa mchezaji raia wa India Yan DHANDA anayecheza ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora toka Asia.
Yan DHANDA anakuwa Muhindi wa kwanza kusajiriwa na Liverpool katika historia ya klabu hiyo na ameonekana mapema tu kua atakuja kua Mchezaji mzuri sana kwa kipaji alichonacho.
Mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu kuwepo klabuni hapo na anakua mchezaji wa kwanza kabisa kusajiliwa na timu kubwa kwa wachezaji wenye asili ya Kihindi na waliochanganyika na wazungu.
DHANDA alizaliwa katika Jiji la Birmingham na kuanza kucheza mpira katika Club ya West Bromwich Albion, lakini alichukuliwa na Liverpool mwaka 2013 akiwa na miaka 17 tu.
Mchezaji huyo amekwisha fanya mazoezi na timu kubwa ya Liverpool mara nyingi tu katika miezi 12 iloyopita na endapo akifanikiwa kucheza katika timu kubwa atakua amejiandikia Historia ya kua Mchezaji wa kwanza wa Kihindi kuichezea Liverpool.
Liverpool inatakiwa kuilipa West Brom kiasi cha £200,000 kwa kumchukua jumla kinda huyo wa Kihindi ambae pia alishinda tuzo ya Mchezaji bora toka ASIA anaecheza England. Pia DHANDA anaonekana atakujakua Mchezaji mzuri sana tena mwenye asili ya Kiasia kuja kua nyota.
#Source_Bin_Slim
LIVERPOOL YASAJIRI MCHEZAJI KUTOKA INDIA
Reviewed by Unknown
on
03:16
Rating:
No comments: