Recent Posts

NEWS: MECK SADIKI: WAFANYAKAZI WA KIGENI WAPEWE SOMO.

MKUU WA MKOA WA DAR- ES SALAAM MECK SADIKI ASEMA WAFANYAKAZI WA KIGENI WAPEWE SOMO.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mheshimiwa Meck Sadiki amewaomba watanzania wanaopata ajira katika kampuni mbalimbali za wawekezaji waliopo nchini wametakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kutisha wawekezaji hao kwa kutofanya kazi kwa bidii,uadilifu na uaminifu.

Meck Sadiki aliyasema  hayo jana jijini dar es salaam wakati akizindua duka kuu la uchumi katika tawi liliopo mbezi, kawe pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa promosheni ya mimi na mwanahisa.

Katika promosheni hiyo Elizabeth Robert mkazi wa kinondoni ndio alikuwa mshindi katika promosheni hiyo,wahisa za uchumi zenye thamani ya shilingi milioni tano baada ya kufanya manunuzi katika tawi la shekilango,Desemba 22 mwaka jana.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa na kusema kuwa wapo baadhi ya watanzania ambao walikuwa wakikatisha tamaa wawekezaji kwa kutokuwa na mahusiano mazuri kazini huku wengine wakidiriki ndugu,ama jamaa zao hata zaidi ya mara moja.

Alisisitiza kuwa watanzania mnapopata kazi lazima zifanywe kwa uadilifu na kuzingatia maadili ya kazi ili kutofikia wakati ambapo mnaweza kuachishwa kazi kwa uzembe,hata hivyo alisema kuwa bahati mbaya watanzania wengi wanatabia ya kusahau.

Katika suala la usalama madukani na maeneo yote yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa,alisema kwamba ni jambo ambalo watanzania 430 wanafanya kazi katika maduka hayo katika matawi mbalimbali.

NEWS: MECK SADIKI: WAFANYAKAZI WA KIGENI WAPEWE SOMO. NEWS: MECK SADIKI: WAFANYAKAZI WA KIGENI WAPEWE SOMO. Reviewed by Unknown on 11:17 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.