Recent Posts

NEWS: CHANZO CHA SHAMBULIO NCHINI UFARANSA: NI KUCHORWA KWA KATUNI YA MTUME MOHAMMED.

Taarifa za uchunguzi juu ya Shambulio la kigaidi nchini ufaransa zimeeleza kuwa ni kutokana na gazeti moja nchini humo kuchora katuni ya mtume mohammed.

Taarifa kupitia vyombo mbali mbali vya habari nchini humo zinaeleza kuwa gazeti la kila wiki la vibonzo la
Charlie Hebdo ndio lililoleta mtafaruku mzima na kupelekea kuzuka kwa shambulizi la kigaidi lililo pelekea watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, ambapo katika toleo la kesho jumatano gazeti hilo linatajia kutoa tena chapisho la kibonzo cha mtume mohammed katika ukurasa wake mbele huku kichwa cha habari kikisema yote yamesamehewa.

Hata hivyo inasemekana kuwa kibonzo hicho cha mtume mohammed kime mwonyesha akishikilia bango lililoandikwa "je suis charlie" maeneo yenye tafsiri ya "mimi ni charlie" ambayo pia ndiyo yaliyotumika kuonyesha mshikimano baada ya shambulio katika ofisi za gazeti hilo jumatano wiki iliyopita ambapo wafanyakazi kumi na wawili wa gazeti hilo waliuawa

Fahamu kwamba kuna nakala zaidi milioni tatu za gazeti hilo tayari zimeandaliwa kuchapishwa kwa ajili ya kesho, ni tofauti na kawaida ambapo huwa linachapisha nakala sitini elfu kwa wiki.

NEWS: CHANZO CHA SHAMBULIO NCHINI UFARANSA: NI KUCHORWA KWA KATUNI YA MTUME MOHAMMED. NEWS: CHANZO CHA SHAMBULIO NCHINI UFARANSA: NI KUCHORWA KWA KATUNI YA MTUME MOHAMMED. Reviewed by Unknown on 00:12 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.