Recent Posts

ICC YAKUBALI PARESTINA KUWA MWANACHAMA WAKE

Umöja wa mataifa umethibitisha kuwa Parestina,itakuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa ya ICC iliyopo chini ya amri ya Roma kuanzia tarehe 1 April mwaka huu.

Hata hivyo kauli hiyo iliyotolewa hivi leo kulingana na taarifa kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa kimataifa Banki Moon iliyochapishwa katika mtandao wa mkataba wa umoja huo

Fahamu kwamba kauli hiyo itawawezesha makundi mbalimbali ya wapiganaji wa kiparestina kushitakiwa endapo itakeuka maadili.

Hata hivyo Raisi wa Parestina Mahmoud Abass alituma maombi ya kujiunga na mahakama ya uhalifu wa kivita wiki iliyopita jambo ambalo lililoikasirisha Israel.

Fahamu kwamba marekani tayari imesitisha fedha za kila mwezi za parestina ambazo ilikuwa ikichukuwa kama kodi kwa niaba yake.

Wiki iliyopita waziri mkuu nchini Israel Benjamini Netanyahu aliyasema hayo kuwa hatokubali wanajeshi wake kufikishwa mbele ya mahakama hiyo.


ICC YAKUBALI PARESTINA KUWA MWANACHAMA WAKE ICC YAKUBALI PARESTINA KUWA MWANACHAMA WAKE Reviewed by Saidia Turuki on 03:56 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.