Recent Posts

MIILI 37 YAPATIKANA KATI YA ABIRIA 162 WALIYOPOTEA NA NDEGE YA AIR ASIA WIKI ILIYOPITA.

Shirika la uokoaji nchini Indonesia limesema kuwa muda mfupi uliopita,kwamba zaidi ya watu 162 waliopotea katika ndege ya Air Asia imepatikana miili 37.

Hata hivyo baadhi ya waokoaji wasema kuwa Helkopta na Meli za kijeshi zimefanya doria katika eneo la bahari, ambapo vitu vya kuchunguzia vinaeleza kuwa mabaki ya ndege,vilionyesha kuwa eneo hilo kwa sasa imetengemaa japokuwa mikondo ya bahari mahali hapo bado pana nguvu.

Baadhi ya vikosi vya wapiga mbizi wa Indonesia na Urusi vina matumaini ya kupata vifaa vya kurekodia mawasiliano ndani ya ndege,ambavyo vitasaidia kujua sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo, iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya kwenda Singapore.

Fahamu kwamba ndege hiyo ilipotea wiki iliyopita ilikuwa na jumla ya abiria 162, na wote walipotea na ndege hiyo mpaka sasa waokoaji na wapiga mbizi bado wanatafuta baadhi ya miili iliyopotea.

MIILI 37 YAPATIKANA KATI YA ABIRIA 162 WALIYOPOTEA NA NDEGE YA AIR ASIA WIKI ILIYOPITA. MIILI 37 YAPATIKANA KATI YA ABIRIA 162 WALIYOPOTEA NA NDEGE YA AIR ASIA WIKI ILIYOPITA. Reviewed by Saidia Turuki on 03:42 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.