Recent Posts

NEWS: MVUA YALETA KILIO KIKUBWA MSUMBIJI.

MVUA YALETA KILIO KIKUBWA MSUMBIJI.

Watu kadhaa Nchini Msumbiji wamepoteza maisha na wengine kupotelewa na ndugu zao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Kupitia vyombo mbali mbali vya habari Nchini humo, Taarifa zinasema kuwa serikali ya msumbiji ilitoa tahadhari ya mafuriko hasa kwenye ukanda wa kaskazini pamoja na katikati mwa Nchi hiyo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha nchini humo.

Fahamu Hadi sasa kuna watoto takribani18 hawajulikani walipo ambapo taarifa zaidi zinaeleza kuwa idadi kubwa ya watu walisombwa na maji yaliyokuwa ya kitiririka katika mto mmoja nchini humo.

Aidha imeelezwa kuwa mawasiliano ya barabara inayounganisha eneo la kati na kaskazini mwa nchi hiyo yameharibika na kukwamisha shughuli za utoaji misaada.

NEWS: MVUA YALETA KILIO KIKUBWA MSUMBIJI. NEWS: MVUA YALETA KILIO KIKUBWA MSUMBIJI. Reviewed by Unknown on 03:34 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.