Recent Posts

MAELFU YA WATU WALIUAWA NCHINI SYRIA 2014.

Katika mwaka 2014 nchini Syria ulikuwa mbaya sana kuliko miaka yote iliyopita,kutokana na migogoro mikubwa iliyotokea nchini humo,na ilidumu kwa miaka 4,na ilipofika mpaka mwaka wa 2014 watu zaidi ya 76000 walipoteza maisha kutokana na vurugu na migogoro iliyokuwa ikiendelea

Shirika la haki za binadamu Observatory lenye makao yake nchini uingereza,lilisema kuwa katika mgogoro huo kati watu waliouawa jumla yake ni 17790 watoto walikuwa 3501 nchini humo.

Wakati huo huo zaidi ya watu 15000 walikufa katika mgogoro wa Iraq mwaka 2014,idadi hiyo ilifanya na kuonyeaha kuwa mwaka huo ulikuwa mbaya sana nchini Syria kuliko miaka yote katika mgogoro wa Iraq tangu mwaka 2007.

Mauaji hayo yalitokana na kuongezeka kwa harakati za kundi la Islamic state na makundi mengine ya wapiganaji katika nchi hiyo ya syria na Iraq.

Lakini katika mgogoro huo kulikuwa na mashambulio ya anga yaliyokuw yakiongozwa na marekani dhidi ya Islamic state,( IS) yaliyopigana dhidi ya majeshi ya serikali na waasi wa nchini Syria kutokana ghasia za kidini zilizokuwa zikiendelea na kusababisha idadi kubwa ya vifo vilivyotokea.

Mashambuliö ya anga yaliendelea mpaka Alhamisi 17 mwaka 2014 yalilenga maeneo ya IS karibu na miji ya Ragga, Kobane na Deir al -zour nchini syria.

MAELFU YA WATU WALIUAWA NCHINI SYRIA 2014. MAELFU YA WATU WALIUAWA NCHINI SYRIA 2014. Reviewed by Saidia Turuki on 02:03 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.