Wafanyakazi mbalimbali zaidi ya 81 kutoka
Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo tayari wamewasili nchini Guinea ili
kusaidia kukabiliana na gonjwa la hatari la Ebola ambalo linasumbua
sana.
Wafanyakazi hao wa afya ni pamoja na kundi la madaktari na wauguzi,wataalamu wa maabara na wa saikolojia na mawasiliano.
Hata hivyo jopo hilo la wataalamu mbalimbali baada ya kufika nchini muda mfupi uliopita,wataanza kazi moja kwa moja katika vitendo husika na kutibu ugonjwa huo wa Ebola.
Fahamu kwamba watabibu hao wamesema kuwa watatoa mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wa mitaa ya nchi hiyo kuhusu namna ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola nchini humo.
Wakati huohuo shirika la Afya Duniani limetoa takwimu mbalimbali na mpya za mlipüko wa Ebola kwa mujibu wa shirika hilo,vifo vilivyotokana na ebola katika nchi tatu zilizoathirika zaidi ya watu 8000
Hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa nchi ya Sierra Leone ilikuwa na wagonjwa 9771 na vifo 2915, nchi ya Liberia ilikuwa na wagonjwa 8115 na vifo 3471 ambapo nchi ya Guinea imeripotiwa kuwa na wagonjwa 2769 na vifo 1767.
Takwimu hizo za magonjwa na vifo ya Ebola ni hadi kufikia Desemba 31 kwa upande wa Liberia na upande wa nchi za Siera Leona na Guinea takwimu hizo ni hadi January 3 mwaka huu 2015.
Fahamu kwamba mpaka sasa kuna taarifa za wagonjwa wa Ebola 8 nchini mali na vifo vya watu 6, ambapo uingereza ina mgonjwa mmoja na hakuna aliyepoteza maisha.

EBOLA YAPATA KIBOKO YAKE KUTOKA GUINEA.
Reviewed by Saidia Turuki
on
07:27
Rating:
No comments: