Recent Posts

NEWS: RAISI KIIR AUGUA GHAFLA NA KUCHELEWA KATIKA MAZUNGUMZO.

RAISI KIIR AUGUA GHAFLA NA KUCHELEWA KATIKA MAZUNGUMZO.

Raisi Kiir aligua gafla na kuchelewa katika mkutano na viongozi wa kikanda uliokuwa umeandaliwa ili kujadili mgogoro wa mwaka mmoja unaotokota nchini Sudani Kusini kufuatia kucheleweshwa baada ya Raisi salva kiir kuugua na kukimbizwa hospitali mjini Addisi Ababa nchini Ethiopia.

Afisa mmoja wa shirika la " IGAD" ambalo linafanya juhudi za kuwakutanisha viongozi wa sudani kusini kwa lengo la kumaliza vita,aliiambia BBC kwamba Raisi Kiir alianza kuvuja damu kutoka puani, ambapo kabla ya kuugua jana alifanya mazungzo na kiongozi wa waasi Riek Marshar na kumtaka kiongozi huyo kupuuzia mbali maswala yanayochochea mgogoro huo ili kumaliza mgogoro huo ambao umedumu kwa mwaka mmoja.

Swala kuu kwenye ajenda ni kusuluhisha maswala yanayoleta kizungumkuti kuhusu serikali ya muungano kama moja ya suluhu la kupatikana amani, ambapo Katika hatua hiyo pande zote zinazozozana zilikosa kufikia makubaliano kuhusu wadhifu wa waziri mkuu na ikiwa anapaswa kuwa na mamlaka kuu.

#Fahamu Maelfu ya watu walifariki na wengine zaidi ya milioni moja kuachwa bila makao tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe kuzuka nchini humo Desemba mwaka 2013.

 
NEWS: RAISI KIIR AUGUA GHAFLA NA KUCHELEWA KATIKA MAZUNGUMZO. NEWS: RAISI KIIR AUGUA GHAFLA NA KUCHELEWA KATIKA MAZUNGUMZO. Reviewed by Unknown on 06:22 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.