Recent Posts

GERRARD AIPA LIVERPOOL MKONO WA KWAHERI,

>>Kapten wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard amethibitisha kuondoka katika klabu hiyo mara baada ya msimu huu kumalizika na kujiunga na ligi kuu nchini Marekani MLS.

Gerrard amesema hayo na kukiri kuwa ni maamuzi magumu aliyoyachukua kwa kuiacha timu aliyipenda tangu utotoni ila imebidi kufanya hivyo.

Gerrard alisisitiza kuwa anaondoka Liverpool ila hatojiunga na timu ambayo baadae inaweza kukutana na timu yake ya zamani.

Gerrard alianza kuichezea Liverpool mwaka 1998 na sasa anachuliwa kama mfalme wa klabu hito kutokana na msaada wake mkubwa alioutoa kwa timu hiyo.

Akiwa Liverpool Gerrard amefanikiwa kuchukua tunzo za mchezaji bora mbalimbali, na vikombe kama UEFA CUP, UEFA CHAMPIONS, FA CUP mara mbili, Carring Cup mara 3, UEFA SUPER CUP mara 2

GERRARD AIPA LIVERPOOL MKONO WA KWAHERI, GERRARD AIPA LIVERPOOL MKONO WA KWAHERI, Reviewed by Saidia Turuki on 04:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.