Recent Posts

NEWS: KIBONZO CHA MTUME MUHAMMAD CHA SABABISHA KUCHOMWA KWA MAKANISA NIGER.

KIBONZO CHA MTUME MUHAMMAD CHA SABABISHA KUCHOMWA KWA MAKANISA NIGER.

Waislam katika nchi mbalimbali wametokea kuguswa na kuumizwa na tukio la kuchapishwa kwa kibonzo cha Mtume Muhammad nchini ufaransa wiki mbili zilizopita katika gazeti la #Charie_Hebdo huku wengine wakiandamana na kusababisha mazara mbalimbali sehemu tofauti tofauti, ili kulipiza kisasi kwa wahusika wa tukio la kumchora mtume wao Muhammad.

Taarifa mbali mbali zilisema kuwa Watu 5 wameuawa kwenye mji mkuu wa Niger,Niamey siku tatu zilizopita kutokana na maandamano ya kupinga kuchapishwa kwa kibonzo cha Mtume Muhammad kupitia gazeti la kila wiki nchini Ufaransa la Charlie_Hebdo.

Taarifa zaidi zinadai kuwa tukio hilo ambalo bado linaendelea nchini Niger la maandamano, lime husisha vijana wapatao 1000 ambao miongono mwao walionekana wame beba vyuma huku wengine wakibeba mashoka, ambapo imeelezwa kuwa waliungana kwa pamoja na kuandamana kwenye barabara za mji huo ndipo walipo anza kuwarushia polisi mawe, polisi ambao walikuwa wakituliza ghasia za waandamanaji kwa kuwarushia mabomu ya machozi.

Aidha imedaiwa kuwa waandamanaji nchini humo walichoma takribani makanisa 7 katika mji wa Niamey, huku maandamano yalivyozidi kuendelea zilionekana maiti 2 zilizokatwakatwa zilizo daiwa kuwa huenda zikawa za watu kutoka katika kanisa moja lililoteketea kwa moto nchini humo.

Hata hivyo watu waliokuwepo majumbani mwao wali pata kushihudia maandamano hayo kupitia runinga za vyombo mbali mbali vya habari na kudai kuona waandamanaji wakirarua Biblia huku wakisema Allahu Akbar na kupeperusha Koran juu.

 
NEWS: KIBONZO CHA MTUME MUHAMMAD CHA SABABISHA KUCHOMWA KWA MAKANISA NIGER. NEWS: KIBONZO CHA MTUME MUHAMMAD CHA SABABISHA KUCHOMWA KWA MAKANISA NIGER. Reviewed by Unknown on 08:41 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.