Recent Posts

MAHUSIANO YA NDOA YANUKIA KATI YA JAGUAR WA KENYA NA IRENE UWOYA WA BONGO.

Msanii wa muziki na mshindi wa tuzo mbili kubwa za
muziki nchini Kenya # Pearl_of_Africa_Music_Award
kupitia kipengele cha best male artist in Kenya na
tuzo ya # Kisima_Music_Award katika kipengele cha
Best Boomba artist, Charles Njagwa Kanyi "Jaguar"
amewaacha wa #Tanzania midomo wazi kutokana
na kueleza ya moyoni juu ya hisia zake kwa Msanii
wa Bongo movies kutoka Tanzania, Irene Uwoya
na kuthubutu kujieleza kuwa amejipanga kuja
Tanzania mwishoni mwa mwaka huu
kuja kumuona staa huyu anayevutiwa naye na
kuwaona wazazi wake pia.

Jaguar kupitia kipindi cha E-Newz cha Eatv alisema
kuwa akija Tanzania
hataishia kumuona Irene tu, bali atakwenda
hadi kwa wazazi wa staa huyu kwa lengo ambalo
hakulifafanua kiundani.
“Mimi naona nitue Tanzania, sijui nije December,
sijui nimuijie Irene Uwoya, nije kumchukua,
mwambie naja kumchukua, ameniambia nione
wazazi kwanza, naja December kumchukua,”
alisema Jaguar wakati akihojiwa.

Kwa upande wa staa wa filamu hapa nchini Irene
Uwoya alipo hojiwa na # Bongo5_Media juu ya safari
ya #Jaguar kuja Tanzania kwa ajili yake alikili kuwa
anakuja kwa ajili ya mipango yao ya harusi.

“Tunampango wa kuoana, bado anakuja,” alisema
Irene Uwoya huku akicheka.

# Fahamu pia kuwa Irene Uwoya alisha wahi kuwa na
mahusiano ya ndoa na mchezaji mpira raia wa
Rwanda Hamad Ndikumana "Kataut" ambaye
walifunga naye ndoa mwaka 2008 na kujaliwa mtoto
anaye itwa # Dagrei_Krish licha ya kuwa na skendo
za kutoka na msanii wa bongo fleva Nasibu Abdul Diamond Platnumz

MAHUSIANO YA NDOA YANUKIA KATI YA JAGUAR WA KENYA NA IRENE UWOYA WA BONGO. MAHUSIANO YA NDOA YANUKIA KATI YA JAGUAR
WA KENYA NA IRENE UWOYA WA BONGO. Reviewed by Unknown on 06:56 Rating: 5

4 comments:

  1. Huyo demu nae cheche 2 hana lolote

    ReplyDelete
  2. Fala wa mapenzi huyo! Haja waona wengine kaja kupapatikia bomu

    ReplyDelete
  3. Nyinyi hamjui tu huyo kapenda hapo eheee!

    ReplyDelete
  4. Mapenzi kizungu zunguz

    ReplyDelete

Powered by Blogger.