BAADA ya kuwasili jana kutoka nchini Brazil,
kiungo mkabaji Emerson de Oliveira Neves
Roque leo ameanza mazoezi mepesi asubuhi
katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola
jijini Dar es Salaam kufuatia kusaifri kwa zaidi
ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro .
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa
Yanga katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni
siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania
na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya
kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na
kutoa uchovu wa safari.
Fahamu Kiungo huyo
alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso
FC iliyopo ligi daraja la pili nchini Brazi katika jiji
la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikuwa
akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland
kwenye klabu ya Piotrkow Trybunalski FC .
Sababu ya mchezaji huyo kufanya mazoezi mepesi, Kocha Mkuu wa Yanga , Marcio Maximo
amesema mchezaji huyo leo alikuwa na
programu ya mazoezi mepesi kutokana na
uchovu wa safari ila kesho anatarajiwa
kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana
na ratiba iliyopo .
Fahamu pia Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi
benchi la ufundi kumsajili basi moja kwa moja
ataingia makubaliano na klabu hiyo kwa ajili ya
kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara .
(Pichani Kiungo Mbrazil Emerson de Oliveira wa pili
kutoka kulia, akiwa mazoezini leo asubuhi
katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola ,
Dar na wengine ni Hamis Kiiza , Hussein Javu na
Coutinho)
credits:GPL and Yanga Sc.
Simba mpoooo!!
ReplyDeleteTupo we boya!
ReplyDelete