Baada ya msanii Amini Mwinyimkuu kuagwa rasmi THT kampuni mpya inayomsimamia muimbaji huyo imetaja kiasi cha pesa ambacho kitahusika kwa ajili ya kuanza
kumsimamia baada ya kuingia naye mkataba rasmi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni BME inayomsimamia
Amini aitwaye Newton, amezungumzia jinsi
walivyojipanga kumsimamia msanii huyo ambaye
alilelewa na THT kwa miaka 10, ambapo alisema kuwa
wamepanga kumfanyia kazi nzuri za kumuendeleza
kimuziki, kuanzia kufanya audio nzuri pamoja na kufanya video nzuri ikiwa ni pamoja na kumtangaza kimataifa.
" kwa mfano
kwenye video tunajua soko la video sasa hivi ni
soko ambalo lina ushindani sana, kwahiyo tutakuwa
tunaendana na ushindani wa kidunia.” alisema
Newton kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Newton pia aliongezea kuwa fungu walilotenga kuanzia
usimamizi wa Amini ni shilingi milioni 48.
“Kwa Amini tumeamua kwanza kuweka millioni 48
lakini so far sasa hivi tumetenga fungu la millioni 30
ambalo tumeshaanza kulitumia mpaka sasa. muziki
una mambo mengi kuna video, kuna audio kuna
social network, pia kuna maisha yake Amini
anatakiwa aishi anatakiwa avae ni mambo mengi na
nadhani hata hiyo hela yenyewe itafikia kipindi
itabidi tuongeze kutokana na mahitaji.”
No comments: