Recent Posts

ABIRIA WA SHUKA NA KUSUKUMA NDEGE ILIYO NASA.

Si kitendo cha ajabu sana bali ni matumizi ya
jitihada na nguvu pia na kujitoa na siku zote
nikawaida kwa Usafiri wowote endapo ukikutana na
janga lolote la hitilafu inayo pelekea kutotembea
kwa usafiri huo na kulazimu watu ama abiria
kuusukuma, mfano Gari dogo, basi ama hata pikipiki
lakini ni kwa mara chache sana kusikia kitendo
kama hicho kwenye usafiri wa anga yaani ndege.

Raia huko nchini Urusi wamelazimika kushuka na
kusukuma ndege iliyokuwa imekwama katika theluji
kufuatia baridi kali katika uwanja wa ndege wa IGARKA_Airport uliopo Urusi katika mji wa
Siberia kufuatia usafiri wao huo wa anga kunasa
katika theluji huku chanzo kamili kikidaiwa kuwa ni
mafuta ya breki yaliyo pakwa ambayo haya kuweza
kustahimili baridi kali lililokuwa na kiwango cha
nyuzi joto 52c na kupelekea breki za ndege hiyo
kuganda hivyo kushindwa kutembea na kunasa
kwenye theluji.

Ndege mali ya kampuni ya  U_Tair yenye uzito wa
tani 30 ililazimika kusukumwa na abiria wapatao 70
ambao walishuka kuisukuma kufuatia pia jitihada
zilizo tumiwa na kampuni hiyo za kutumia trecta
kuivuta kushindwa kuzaa matunda hivyo kulazimu
wingi wa abiria hao ambao takribani wote walikuwa
ni wanaume ambao wanadaiwa kuwa ni
wafanyakazi wa kampuni za gesi na mafuta ambapo
katika jitihada zao waliisukuma kinyume nyume na
kufanikiwa kuitoa ndege hiyo.

Taarifa kamili zinaeleza kuwa ndege hiyo haikuwa
na hitilafu yoyote isipokuwa baridi kali iliyo
ambatana na theluji ndio iliyo ikwamisha ndege hiyo
ya U_Tair lakini baada ya jitihada za kusukumwa
iliweza kunasuka na kuendelea na safari ambapo
ndege hiyo ilitua salama katika mji mkuu wa
Krasnoyarsk .

ABIRIA WA SHUKA NA KUSUKUMA NDEGE ILIYO NASA. ABIRIA  WA SHUKA NA KUSUKUMA
NDEGE ILIYO NASA. Reviewed by Unknown on 00:51 Rating: 5

2 comments:

Powered by Blogger.