Recent Posts

YALIYO JILI JANA,BUNGENI JUU YA SAKATA LA TEGETA ESCROW.

Hali ya sintofahamu ilizidi kutokea juu ya suala la akaunti
ya Tegeta Escrow ambapo siku ya Jana asubuhi Mh. Anna Makinda
alisema Wabunge wasiwe na wasiwasi suala
litajadiliwa hakuna wa kuingilia, lakini kufikia jioni
mahakamani ilitoa amri juu ya suala hilo kutokujadiliwa kwa
sasa kitendo ambacho kimezidi kuwachanganya wa Tanzania walioguswa na sakata hilo la utaifishaji wa Fedha hizo za wananchi ambazo zinadaiwa kuchotwa
toka kwenye akaunti hiyo na vigogo mbalimbali
wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Majaji wa mahakama
kuu na Viongozi wa dini.

Lakini wakati mambo yalivyo endelea Bungeni:

TUNDU LISSU AMEFUNGUKA NA
KUSEMA FEDHA HIZI NI ZA NCHI NA MUHONGO
AMESEMA UONGO.

Lissu: Naomba niseme kuwa Bunge lako
limepotoshwa moja kwa moja na Mh. Muhongo

Lissu: Kiambatanisho namba 2 sio ushahidi wa
standard charted Hong Kong kutambua chochote ila
ni hati ya madai.

Lissu: Vitambulisho viwili alivyoleta Muhongo ni kesi
za mahakama kuu za mwaka huu, hazina ushahidi
wowote wa tuhuma zake

Lissu: Kwa ushahidi wa taarifa ya kamati na CAG hizi
ni pesa za umma, kama zisingekuwa za umma Rais
asingeelekeza zilipwe

Lissu: Inakuwaje pesa za binafsi zitolewe maamuzi
na Rais, Mawaziri, na Magavana?

Lissu: PAP waweze kupewa hizi pesa ilibidi wapewe
kibali na Waziri Muhongo, lakini haijapata usajili hivyo
si kampuni halali.

Lissu: Ndani ya siku moja zimetoka bilioni 78, na
kama fedha zinazodaiwa ni binafsi kwanini wapewe
Viongozi wa Umma na dini?

Lissu: Kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kuwa
hizi ni fedha za umma. TRA, TAKUKURU na CAG
wamekiri ni fedha za umma

Lissu: Rushwa tupu imetambaa hadi mahakamani,
Majaji wanapewa fedha tukiuliza mnasema ahahahha.

Lissu: Waziri Mkuu, Tibaijuka , Muhongo na wote
waliotajwa walioko humu ndani, tuanze nao maana
hawa tunawaweza

Lissu:Kuna la kusisitizwa hapa kuhusu BOT,Benki
kuu ni huru na haiwezi ikajificha nyuma ya ushauri
mbovu wa Mwanasheria mkuu.

Lissu: TRA pekee ndio chombo kikuu chenye
mamlaka hapa nchini kutoa ushauri juu ya ushuru upi
wa kodi ulipwe

Lissu: Mwanasheria Mkuu sio mshauri mkuu wa
maswala ya kodi hapa nchini ila TRA.

Lissu: Kamati inasema Waziri Mkuu awajibike
kwakuwa ndiye mwajibikaji mkuu wa shughuli za
serikali, hii ni sahihi kabisa.

Lissu: Tunamwachaje Waziri wa wizara ya fedha
ambaye ndiye mhusika mkuu wa masuala ya fedha?

Lissu: Mkuu wa Kitengo cha Financial Intelligence
Unit ndani ya Wizara ya Fedha anatakiwa kuwajibika

Lissu: Leo yametokea yaliyozungumzwa toka mwaka
1994 kuwa IPTL itakuja kutuumiza

Lissu: Tunataka fedha zetu zirudi maana leo haya
yanatokea Jakaya Kikwete ndiye Rais wa nchi

Lissu: Wakati IPTL inakuja, Rais Kikwete alikuwa
Waziri wa Nishati na Madini, wakati wanasaini
mkataba alikuwa Waziri wa Fedha

Lissu: Hakuna jambo baya kama Hakimu kupewa
milioni 400, na hiyo sio dhihaka ila ni wajibu wetu
kuyasema haya.

Lakini pia katika utetezi wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa:

PESA ZA ESCROW SI ZA
UMMA.

Taarifa zaidi kutoka Bungeni zinasema kuwa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
kwa niaba serikali alitoa taarifa yake ya utetezi
kuhusu sakata la ESCROW na kusema kuwa pesa
zilizokuwa katika Akaunti ya Tegeta ESCROW zote
zilikuwa ni za IPTL na siyo za UMMA, na kwamba
bado TANESCO inadaiwa zaidi ya Bilion 354 na
makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo Bilion 94
za IPTL.

Nini maoni yako Mtanzania uliyeguswa na sakata hili?!.

YALIYO JILI JANA,BUNGENI JUU YA SAKATA LA TEGETA ESCROW. YALIYO JILI JANA,BUNGENI JUU YA SAKATA LA TEGETA ESCROW. Reviewed by Unknown on 19:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.