>>TIMU ya Argentina imepangwa pamoja na Uruguay
katika Kundi B kwenye michuano ya Copa America
mwakani, 2015.
Droo hiyo pia imezikutanisha Colombia na wenyeji wa
Kombe la Dunia 2014, Brazil. Michuano hiyo
itakayofanyika nchini Chile, itashuhudia timu hizo
mbili za Amerika Kusini zikikutana tena kwa mara
nyingine, baada ya kukutana mara mbili hivi karibuni.
Brazil iliitoa Colombia katika Robo Fainali ya Kombe
la Dunia Julai, kabla ya Neymar kufunga bao la
ushindi katika mechi ya kirafiki baina ya mataifa hayo
mawili Septemba.
Nyota wa Barcelona, Lionel Messi ataiongoza
Argentina kwenye Copa America ambako
wamepangwa pamoja na Uruguay ya Suarez
Mchezo huo unatazamwa kuwa wa kuvutia kutokana
na wachezaji hao kuchezea klabu moja ya FC
Barcelona.
Makundi ya Copa Amerika 2015 yako hivi;-
KUNDI A: Chile, Mexico, Ecuador, Bolivia
KUNDI B: Argentina, Uruguay, Paraguay, Jamaica
KUNDI C: Brazil, Colombia, Peru, Venezuela.
RATIBA YA COPA AMERICA HATUA YA MAKUNDI:
JUNI 11 - Chile v Ecuador (Kundi A)
JUNI 12 - Mexico v Bolivia (Kundi A)
JUNI 13 - Uruguay v Jamaica (Kundi B)
JUNI 13 - Argentina v Paraguay (Kundi B)
JUNI 14 - Colombia v Venezuela (Kundi C)
JUNI 14 - Brazil v Peru (Kundi C)
JUNI 15 - Ecuador v Bolivia (Kundi A)
JUNI 15 - Chile v Mexico (Kundi A)
JUNI 16 - Paraguay v Jamaica (Kundi B)
JUNI 16 - Argentina v Uruguay (Kundi B)
JUNI 17 - Brazil v Colombia (Kundi C)
JUNI 18 - Peru v Venezuela (Kundi C)
JUNI 19 - Mexico v Ecuador (Kundi A)
JUNI 19 - Chile v Bolivia (Kundi A)
JUNI 20 - Uruguay v Paraguay (Kundi B)
JUNI 20 - Argentina v Jamaica (Kundi B)
JUNI 21 - Colombia v Peru (Kundi C)
JUNI 21 - Brazil v Venezuela (Kundi C)
By_Sports_Admin_Emmanuel_Senny
No comments: