Recent Posts

YALIYOJILI BUNGENI: KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW!

KUANZIA KWA WAZIRI MKUU

Kamati imesema imejiridhisha pasipo
mashaka kuwa, Waziri Mkuu, Mh.Mizengo Pinda alikuwa ana
taarifa zote kuhusiana na mchakato mzima wa
kuchotwa fedha kutoka katika akaunti ya
ESCROW.

Kamati pia kwa kuzingatia kielelezo namba 22,
inathibitisha bila shaka kwamba, Waziri Mkuu
alikuwa analijua jambo hili vizuri na kwamba
aliridhia muamala huu ufanyike na Ndiyo maana
katika maelezo yake ya Bungeni mara kadhaa
Waziri Mkuu alithibitisha kuwa fedha za
Escrow hazikuwa fedha za Umma.

Ripoti imesema ni jambo la kushangaza kuona
kwamba, jambo kubwa na zito kama hili
lingeweza kufanyika bila ya mamlaka za juu,
hususan Mhe. Waziri Mkuu kufahamu.

Imeongeza kuwa kwa uzito na unyeti wa jambo
hili, vyovyote vile, Waziri Mkuu anapaswa
kuwajibika kwa kauli zake na kwa
kutokutekeleza wajibu wake wa kikatiba
ipasavyo, ili kurejesha imani ya wananchi kwa
serikali yao na viongozi wao wa kisiasa.

MWANASHERIA MKUU

Kwa upande wa mwanasheria Mkuu, Jaji
Fredrick Werema Kamati imethibitisha kuwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali alitoa ushauri ulioipotosha Benki
Kuu ya Tanzania kuhusiana na hukumu ya Jaji
Utamwa J. Kwa kutumia madaraka yake
vibaya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliagiza
kodi ya Serikali yenye thamani ya shilingi 21
bilioni isilipwe 107 na hivyo kuikosesha
Serikali mapato adhimu.

-Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kujua na
kwa makusudi alilipotosha Bunge na Taifa
kwamba mgogoro uliopelekea kufunguliwa
kwa Akaunti ya ESCROW ulikuwa ni mgogoro
wa Wanahisa wa IPTL badala ya mgogoro kati
ya TANESCO na IPTL ambapo Kamati imependekeza
kuwa uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali
utenguliwe mara moja na kisha afikishwe
mahakamani kwa matumizi mabaya ya Ofisi
yaliyopelekea Serikali kupoteza mabilioni ya
fedha.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

Pia Kamati imethibitisha kuwa Waziri wa Nishati na madini Prof. Sospeter
Muhongo amekuwa, mara kwa mara,
akilipotosha Bunge tukufu na Taifa kwa ujumla
kuhusiana na Fedha za Akaunti ya Tegeta
ESCROW kwamba ndani ya fedha hizo
hakukuwa na fedha za umma ambapo alidai Hata mtu wa
kawaida angeweza kujua kwamba washirika
wa ‘Tegeta Escrow Account’ ni akina nani na
masharti ya kutoka kwa fedha hizo kwenye
akaunti ni yapi kwa mujibu wa Mkataba wa
uendeshaji wa akaunti hiyo.

Hata hivyo, katika hali ya kushangaza
kwa makusudi ama kwa sababu anazozijua
vizuri zaidi mwenyewe, Waziri wa Nishati
alinukuliwa kwenye kumbukumbu rasmi za
Bunge, Kwa nguvu
kubwa na kwa kujiamini, akitetea uchotwaji wa
fedha hizo kinyume na masharti ya Mkataba
wa Escrow.

Aidha, Kamati imebaini kuwa Waziri wa
Nishati na Madini ndiye alikuwa dalali mkuu
aliyewakutanisha Bwana Harbinder Singh Sethi
na Bwana James Rugemalira, tena katika ofisi
ya Umma; na pengine hii ndiyo iliyokuwa
sababu ya upotoshaji huu.

Taarifa zinadai kuwa Waziri wa Nishati na
Madini alifanya udalali huo akijua dhahiri kuwa
Bwana Sethi hana uhalali wa kisheria kufanya
biashara kwa jina la IPTL.

Imedaiwa kuwa iwapo Waziri wa Nishati na Madini angetimiza
wajibu wake ipasavyo, Fedha za Tegeta
ESCROW zisingelipwa kwa watu wasiohusika,
na Nchi ingeweza kuokoa mabilioni yaliyopotea
kama kodi za VAT, Capital Gain Tax na Ushuru
wa Stempu ambazo ni sawa na takribani
shilingi bilioni 30.

Hata hivyo Kamati imependekeza kuwa Mamlaka yake ya
uteuzi itengue uteuzi wa Waziri wa Nishati na
Madini kutokana sababu hizo zilizoelezwa.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI

Pia Kamati imethibitisha kuwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini alisema uongo Bungeni kwa
kutamka kauli ambazo zilizokuwa na lengo la
kupotosha umma kuhusu akaunti ya Tegeta
ESCROW ikiwemo kutoa kauli ambazo
zingeweza kusababisha Nchi kuingia kwenye
mgogoro wa kidiplomasia na
nchi ya Uingereza.

Ambapo moja kwa moja Kamati imependekeza kuwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini achukuliwe hatua kali za
kinidhamu ikiwemo kutenguliwa uteuzi wake.

Kamati pia inapendekeza kuwa Naibu Waziri
huyu afikishwe mbele ya Kamati ya Bunge ya
Maadili ili aadhibiwe kama Mbunge kwa
kusema uwongo Bungeni ili liwe fundisho kwa
wabunge wengine kuhusiana na kauli
wanazotoa ndani ya Bunge tukufu.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA NISHATI NA
MADINI

Kamati imethibitisha kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini aliingia
makubaliano ya kutoa fedha katika Akaunti ya
Tegeta ESCROW bila kujiridhisha kikamilifu
kuwa maamuzi ya hukumu ya ICSID 2 yalikuwa
bado kutolewa na hivyo kusababisha fedha
kutolewa bila kukokotoa upya gharama za
‘capacity charges’, jambo ambalo limesababisha
kupoteza fedha za umma.

Viile vile unaambiwa kuwa Kamati imebaini kuwa, Katibu Mkuu
hakufanya uchunguzi wa kina (due diligence)
kujiridhisha uhalali wa Kampuni ya Mechmar
kuuzwa kwa Piper
-Kwa maana hiyo, Katibu Mkuu, Wizara ya
Nishati na Madini, pengine kwa uzembe wake
ama kwa kukusudia kwa sababu anazozijua
yeye mwenyewe zaidi, amesaidia uchotwaji na
hatimaye utakatishaji wa fedha haramu.

Kamati pia imethibitisha uzembe wa hali ya
juu uliofanywa na Katibu Mkuu huyo,
kushindwa kujiridhisha kama masharti ya
Sheria ya kodi ya Mapato Sura ya 333, Kifungu
cha 90(2) yalitekelezwa.

Kifungu hicho
kimsingi kinaitaka mamlaka ya ‘approval’’ ya
uhamishaji wa Makampuni kutotambua
Kampuni mpaka kwanza kodi za uhamishaji
ziwe zimelipwa na hati za malipo ya kodi
zimetolewa na mamlaka ya kodi.
-Kamati inapendekeza kuwa uteuzi wa Katibu
Mkuu huyu utenguliwe, na TAKUKURU
wamfikishe mahakamani mara moja, kwa
kuikosesha Serikali Mapato, matumizi mabaya
ya ofisi na kusaidia utakatishaji wa fedha
haramu.

YALIYOJILI BUNGENI: KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI MKUU, MWANASHERIA MKUU, WAZIRI WA NISHATI NA MADINI WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA TEGETA ESCROW! YALIYOJILI BUNGENI: KAMATI YA PAC YAMTAKA WAZIRI
MKUU, MWANASHERIA MKUU,
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
WAWAJIBIKE KUHUSU RIPOTI YA
TEGETA ESCROW! Reviewed by Unknown on 10:36 Rating: 5

1 comment:

Powered by Blogger.