Na Emmanuel Senny.
Bibi Mariam Abdallah, mwenye umri wa miaka 60,
mkazi wa Kijiji cha Mnanila, ambaye anadaiwa
kushushiwa kipigo nyumbani kwake na Askari wa
JWTZ,akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Kigoma, Maweni kwa matibabu.
Inadaiwa kuwa Novemba 23 mwaka huu, majira ya
saa tatu usiku, watu wanne waliokuwa wamevalia
sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
walivamia nyumbani kwa bibi huyo wakimtafuta
msichana aliyejulikana kwa jina moja la Editha,
ambaye anadaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi
na mmoja wa wanajeshi hao.
Hata hivyo bibi huyo aliwajibu kuwa hakuwa
anamfahamu msichana huyo na kwamba yeye hana
mtoto wa kike, lakini cha kushangaza mmoja wa
askari jeshi hao alianza kumshushia kipigo mfululizo
kwa mateke na ngumi na kumjeruhi sehemu mbali
mbali za mwili wake hasa maeneo ya usoni na
kumsababishia maumivu makali kiasi cha kulazwa
hospitali.
No comments: