Baada ya Spika wa Bunge kuahirisha Bunge mara
mbili siku ya leo Novemba 29 ili kuipa nafasi
kamati ya PAC iweze kufanya marekebisho ya
maneno yaliyoandikwa kwenye maazimio
yaliyowasilishwa na Kamati ya PAC, Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Zitto Kabwe alitaja majina ya
walioteuliwa na Kamati hiyo kuandika maazimio ya
kuwajibisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow ambapo moja kwa moja aliweza kuwaailisha ujumbe kwa wananchi wa Tanzania juu ya majina hayo kupitia akaunti yake ya Facebook kuwa:
PAC imeteua wafuatao kuingia kamati ya kuandika maazimio ya kuwajibisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow
1.Mwenyekiti
2.Makamu mwenyekiti ama Ismail Aden Rage
3.Khamis Kigwangala
4.Luhaga Mpina
5.Amina Mwidau
Wakati huo huo.
MAKINDA AWASHAURI WABUNGE
KUTORUBUNIWA NA FEDHA KISHA AHARISHA
BUNGE HADI JANUARI 27, 2015.
Makinda: Watu wenye mapesa yao wanaokuja
kuwarubuni humu ndani kataeni mkiendekeza
mchezo huu mtajikuta mko ndani wote
Makinda: Hakuta kuwa na huruma wala kinga ya
Bunge, mtawekwa ndani na ubunge wenu utakwisha,
kuweni makini na hawa matajiri
Makinda: Bunge limeahirishwa hadi Tarehe 27,
January 2015.
Vipi maoni yako Mtanzania?!!.
Wanazingua bwana!
ReplyDelete