Recent Posts

LULU, RICHIE MTAMBALIKE WASHINDA TUZO ZA AMVCA 2016.

IMEKUWA ni nafasi kubwa sana yenye Heshima kwa wasanii Toka Tanzania wakiiwakilisha pia Afrika Mashariki katika Tuzo kubwa za Filamu zikiwa zimelenga kuzipa Ushindi filamu zilizofanya Vizuri kwa kuwa na Ubora wa vitu vyote vinavyo paswa kuzingatiwa katika Filamu hasa za Kiafrika.

Tuzo za African Magic Viewers Choice Awards (AMVCA) 2016 zilizotolewa jijini Lagos, Nigeria ya wiki iliyo pita ambapo Kwenye tuzo hizi Elizabeth ‘Lulu’ Michael na Single ‘Richie’ Mtambalike walishinda tuzo kwa kila mmoja wao kwa tuzo moja moja.

Katika Tuzo hizo Richie ndiye aliyekuwa wa kwanza kushinda tuzo ya filamu ya Kiswahili (Best Indigenous Language Movie/TV Series – Swahili) kupitia filamu yake Kitendawili.
 kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo ameandikia kuwa “Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru watanzania wote kwa kunisupport katika kazi zangu,na kwa wote mlionipigia kura nawashukuru mno sina cha kuwalipa zaidi ya kusema Ahsante kwa wasanii wenzangu ahsanteni huu ni mwanzo mpya,”
 
Kwa upande wa Elizabeth Michael 'Lulu' alifuatia kwa Ushindi wa filamu bora Afrika Mashariki (Best Movie – East Africa) kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu. ambapo pia pasipo kutegemea nyota huyo alijikuta akilia kwa furaha wakati akishukuru kushinda tuzo hiyo hadi kushindwa kuongea.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Lulu aliandika maneno haya "Kwanza ningependa kumshukuru Mungu,kiukweli amekuwa mwema na mwaminifu sana katika maisha yangu
Pili,familia yangu hasa mama angu wamekuwa ni watu WA kuni support sana katika kazi zangu
Tatu,watu wote walioshiriki katika movie yangu ya MAPENZI YA MUNGU...!
Mwisho Nashukuru sana mashabiki zangu na wote mlionipigia kura kiukweli siwezi kuwataja mmoja mmoja lkn nyie ndo mmefanikisha hili..! Nimejifunza kuwa mvumilivu na kutokata tamaa ktk maisha,nimepitia magumu mengi mnayoyajua na mengine msiyoyajua lkn muda wote niliinuka nikashukuru Mungu na kuendelea na Safari,sikujali maneno mabaya ninayosemwa wala kukatishwa tamaa...Juhudi binafsi na kuomba Mungu vimekuwa nguzo yangu kwa kipindi chote...najua bdo wasioamini katika Mimi wapo lkn muda utazidi kueleza...naahidi kuwa sitolewa sifa Bali nitazidi kujituma na kuhakikisha natangaza nchi yangu Kupitia Sanaa yetu...!
#Godwin
#mapenziyaMunguBestMovieEastAfrica)


KWA MATUKIO YA HABARI ZA PAPO KWA PAPO TEMBELEA NA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK m.facebook/KAYSTALLION.TZ
LULU, RICHIE MTAMBALIKE WASHINDA TUZO ZA AMVCA 2016. LULU, RICHIE MTAMBALIKE WASHINDA TUZO ZA AMVCA 2016. Reviewed by Unknown on 23:27 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.