Recent Posts

BABU TALE AJITOLEA KUMSAIDIA CHIDI BENZ BAADA YAKUONA HALI YAKE YA AFYA ILIVYO.


HALI ya kiafya ya Msanii maarufu wa Hip-Hop nchini Tanzania, Rashid Abdallah Makwiro 'CHIDI BENZ' baada ya kuathirika na madawa ya kulevya  kwa kiasi kikubwa imefanya wadau wengi kuwa na mitazamo Tofauti kiasi wengine kudhani kuwa pengine ni muathirika wa virusi vya ukimwi lakini kumbe ni matumizi ya dawa za kulevya ambazo pia zilimfanya awekimya katika muziki baada tu ya kuachia nyimbo aliyo mshilikisha Ay na Diamond-Platnumz 'Mpaka Kuchee'.
Muonekano wa Chidi Benz kipindi cha Nyuma na sasa
Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale amejitokeza kumsaidia msanii huyo ili kuimarisha hali yake ya kiafa ikiwa ni pamoja na kumpeleka kituo kinacho husika na Matibabu ya kuachana na matumizi ya Dawa za Kulevya.

SELFIE: Chidi Benz Babu Tale na Msaniiwa Hiphop Kalapina ambaye pia anaendesha kampeni ya kupinga madawa ya kulevya.
"Kusema ukweli nilipoona picha ile nilipata wasiwasi nikidhani Chid Benzi labda ameungua na maradhi yetu ya sasa, sikuamini kama ni madawa ya kulevya ndiyo yamempelekea hali ile,lakini sikuweza kuamini kesho yake ilibidi nimchukue Chid Benzi na kwenda nae kwenye kituo cha afya na kufanya check up ya mwili mzima, lakini baada ya vipimo kutoka akaonekana yuko poa kabisa ila wakagundua tu ni hayo madawa” alisema Babu tale kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Tv.

#FAHAMU: Babu Tale amefanikiwa kumpeleka Chidi Benzi katika kituo cha Tiba dhidi ya dawa za kulevya cha Huko Bagamoyo Mkoani Pwani cha LIFE&HOPE REHABILITATION ORGANISATION "SOBA HOUSE"
BABU TALE AJITOLEA KUMSAIDIA CHIDI BENZ BAADA YAKUONA HALI YAKE YA AFYA ILIVYO. BABU TALE AJITOLEA KUMSAIDIA CHIDI BENZ  BAADA YAKUONA HALI YAKE YA AFYA ILIVYO. Reviewed by Unknown on 04:10 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.