Recent Posts

SONY WANUNUA HISA ZOTE ZA MICHAEL JACKSON ZILIZOPO KWENYE KAMPUNI HIYO.


MICHAEL Jackson akiwa ni mmoja ya wamiliki wenye share(hisa) katika kampuni ya Sony ATV Music Publishing huku Sehemu yake ikiwa ni asilimia 50% tokea mwaka 1995 alipo fanya ubia na kampuni hiyo.

Kampuni ya Sony imeamua kutangaza kununua sehemu hiyo ya hisa za Hayati wa Muziki wa Pop Michael Jackson kwa dola millioni 750 kwa kuwalipa waangalizi wa kazi zake katika kampuni hiyo pamoja na familia yake kiujumla.

Lengo kuu la manunuzi ya Hisa hizo za Michael Jackson ni kuwa sehemu ya pesa hizo zitatumika kupunguza Madeni ya kifedha yanayo muhusu hayati huyo wa Pop ikiwa pia ni kuhakikisha watoto wake wanapata haki kamili ya kumiliki vitu vya uchumi vya Baba yao.

1995 wakati Michael Jackson ana saini ubiya na Kampuni ya Sony.
Hata hivyo manunuzi hayo yanadaiwa kutojihushisha na Kampuni kuu inayo simamia kazi za Michael Jackson ya Mijac Music kwa makubaliano kuwa kampuni hii itandlea kusimamia na kufanya mauzo ya Michael Jackson kama ilivyo awali isipokuwa tu Sony itakuwa ikimiliki baadhi ya kazi za wasanii ikiwa ni pamoja zile za wakongwe wa zamani kama 'The Beatle' amabao ilikwisha kufanya nao makubaliano ya kimapato tayari.


Enzi za Uhai wake Michael Jackson wakati alipo kuwa na Mgogoro na Kampuni ya Sony.


Paul McCartney wa THE BEATLE akiwa na Michael Jackson

SONY WANUNUA HISA ZOTE ZA MICHAEL JACKSON ZILIZOPO KWENYE KAMPUNI HIYO. SONY WANUNUA HISA ZOTE ZA MICHAEL JACKSON ZILIZOPO KWENYE KAMPUNI HIYO. Reviewed by Unknown on 02:22 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.