WAKATI Label ya
WASAFI CLASSIC BABY chini ya Meneja
Babu Tale na Salaam Sk ikiwa na mikakati ya kuongeza wasanii wengine kama nafasi ya kutoa fursa kwa wasanii wenye vipaji habari njema imekuja kwa wasanii wa kike wenye uwezo wa kufanya Muziki mzuri.
Kupitia mahojiano ya
Babu Tale na Msanii wake
Diamond Platnumz katika kipindi cha Planet Bongo siku ya Jana alifunguka kuwa endapo Msanii
Ruby ambaye ni miongoni mwa wasanii wa kike wanao fanya vizuri nchini asingekuwa katika management ya
THT basi wange mchukua ila kutokana na hilo haiwezekani zaidi ya kutoa Fursa kwa Msanii wa kike ambaye anahisi na aajiamini anauwezo kumpita Ruby basi milango iko wazi na vigzo vyake.
|
Babu Tale akiwa na Diamond Platnumz. |
|
"Tuna mpango wa kuwapata wasanii wa Kike lakini wenye vipaji vya ukweli, Industry yetu ina wanawake wachache, tungepata wanawake wanne au watano" alisema Tale.
"Kwangu mimi kama Ruby angekuwa hayupo THT, au hana management tungemchukua, lakini nasema hivi kama anakuja mwanamke, awe na uwezo kumshinda Ruby au kufanana naye"
|
Ruby anaye tamba na nyimbo ya 'Na Yule'. |
Kwa upande wa Diamond Platnumz ambaye ndiye muanzilishi wa WCB amesema msichana anaye hitajika kwao awe na uwezo wa kuandika Mashairi na kutunga nyimbo zake mwenywe.
|
Baadhi ya Vijana wa kundi la WCB linalo milikiwa na Diamond Platnumz |
#FAHAMU
WCB kwa sasa inafanya vizuri kwa wasanii wawili akiwemo Diamond Platnumz kama msanii mkubwa pia na Harmonize ambaye ana nyimbo mpya aliyo fanya na Diamond
"BADO" pia tayari kunautambulisho wa
Msanii mpya anaye itwa Raymond.
|
RAYMOND Msanii mpya wa WCB. |
TEMBELEA NA LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK hapa++
No comments: