Jambo ambalo mtu akilifanya huona kitu cha thamani kiasi kwamba hataki kuliacha kwa wepesi ni dhahiri kuwa hapo panakitu cha thamani kupita malezo ya kawaida, na pia kiasi kikifikia hivi huwa si pa kufichika tena zaidi ni kuangalia nini kinacho fanya upendo mwingi kuhamia katika kitu hicho.
Msanii
Madee kutoka
Tip-Top Connection ambaye ni miongoni mwa wakongwe wenye historia ya kusisimua katika Muziki wa Bongo Fleva tokea kitambo akianza na Producer mkongwe na mwanzilishi wa Bongo Fleva kwa upande wa Production
P-Funk Majani amezidi kuweka wazi mapenzi yake na jinsi anavyo kubali kazi yake ya muziki kama watu wengine wanavyo zikubali kazi zao.
Nilikutana na Post hii katika Instagram acount ya
Madee ikiwa haina siku nyingi sanaa ya yeye kueleza namna anavyo upenda muziki na jinsi atakavyo acha muziki na ni kwa kipindi kipi?!!.
|
Madee akiwa na Mwanaye Sophy. |
Kwenye Post hiyo Madee aliandika maneno haya
"SIACHI MUZIKI, MPAKA MWANANGU ATAKAPO KUWA NA MWANAE' hapo bila shaka ni dhahiri kuwa kuacha muziki kwa Madee hakuko Karibuni kwa maana ya Leo au Kesho.
|
POST ILIYO NUKULIWA. |
|
Madee akifurahi na Mwane Sophy. |
No comments: