Recent Posts

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS ZANZIBAR ULIOFANYIKA MARCH 20.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha S. Jecha Wakati akitangaza matokeo ya Kura za Urais.
AKITANGAZA Matokeo ya Urais Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mh.Jecha Salim Jecha Mach 21 baada ya kumalizika kwa upigaji kura Machi 20 ikiwa ni uchaguzi wa Marudio baada ya kuhairishwa kwa uchaguzi wa Octoba 25 mwaka Jana.
DK. Ali Mohamed Shein akihutubia baada ya kutangazwa Mshindi wa kiti cha Urais.
Mh. Jecha alimtangaza Dk.Ali Mohamed Shein kuwa ndiye Mshindi wa Kiti cha Urais kufuatia kupata kura Nyingi sana kwa kishindo huku pia akiwaacha wagomba wengine kwa nafasi kubwa ya Idadi ya Kura na Asilimia zake.

Mgombea wa kiti cha Urais Dk. Ali Mohamed Shein wakati akiwasili katika ukumbi wa Bwawani ambapo Tume ya Taifa ilikuwa ikitangazia matoko ya Kura za Urais.
Matokeo ya Uchaguzi wa Urais yakiwa ni mjumuisho wa Majimbo 54 ya kisiwani Zanzibar Tume iliwateuwa wagombea wa vyama 14 vya Siasa  kushiriki katika kinyang,anyio cha kiti cha Urais ambapo kwa Majina na Vyama vyao pamoja na kura na Asilimia walizo pata ni kama ifuatavyo:

MGOMBEA                          CHAMA                                       IDADI       ASILIMIA

1.Khamisi Idd Lila                        ACT-WAZALENDO                   1,225                   0.4%
2.Juma Ali Khatib                         ADA-TADEA                              1,562                   0.5%
3.Hamad Rashid Mohamed           ADC                                           9,734                 3.0%
4.Sais Soud Said                           AFP                                               1,303                   0.4%
5.Ali Khatib Ali                             CCK                                             1,980                   0.6%
6.Dk.Ali Mohamed Shein              CCM                                              299,982              91.4%
7.Mohammed Masoud Rashid       CHAUMA                                  493                    0.2%
8.Seif Sharif Hamad                      CUF                                             6,076                    1.9%
9.Tabu Mussa Juma                      D-MAKINI                                 210                      0.1%
10.Abdallah Kombo Khamis           DP                                                512                       0.2%
11.Kassim Bakari Aly                     J-ASILIA                                    1,470                    0.4%
12.Seif Ali Iddi                               NRA                                              266                       0.1%
13.Issa Mohamed Zonga                SAU                                             2,018                    0.6%
14.Hafidh Hassan Suleiman             TLP                                            1,496                    0.5%

 Aidha kwa Mujibu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC):
Idadi ya Wapiga Kura; 503,580
Kura Halali; 328,327 sawa na aslimia; 96.0%
Kura Zilizoharibika; 13,538 sawa na asilimia; 4.0%
Jumla ya Kura zote; 341,865 sawa na asilimia 67.9%
 Kama Tume ilivyo weza kumtangaza Mh.Dk Ali Mohamed Shein kuwa ndiye Rais na huku akiwa Rais aliyekuwa Madarakani katika awamu ya Urais iliyopita.
#FAHAMU. Dk.Shein anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatano tarehe 23 Machi mwaka huu.
MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS ZANZIBAR ULIOFANYIKA MARCH 20. MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS ZANZIBAR ULIOFANYIKA MARCH 20. Reviewed by Unknown on 14:45 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.