Kwenye tukio la kipekee ambalo halikuweza kunaswa na Waandishi wa Habari isipo kuwa Raia wa Kawaida ambaye aliweza kushare picha ya tukio la kipekee ambapo kama sio kufanya hivyo huenda lisinge julikana kwa watu kuwa Rapa Lil Wayne alikatisha safari yake ilikuweza kusalimiana na kuongea na wanajeshi wa Jeshi la Marekani wakati wakiwasili katika kiwanja cha ndege cha Indianapolis International Airport.
Tukio hilo lilikuja wakati Lil Wayne anaondoka na ndege yake ya kukodi kwenye kiwanja hicho cha ndege ambapo inadaiwa aliona wanajeshi wanashuka kwenye ndege yao na hivyo kumuamrisha rubani wake kutopaisha ndege hiyo ili akaonane na wanajeshi hao.
Kupitia Facebook moja ya wafanyakazi wa Uwanja huo wa Ndege Amanda Cooper Lickliter ali fafanua namna tukio lilivyo kuwa na kueleza kuwa Wayne alikuwa akisalimiana pamoja na kupiga picha na Wanajeshi hao wa Marekani wanao kadiriwa kuwa 30.
Kwa upekee wa Tukio hilo indaiwa kuwa kama kungekuwa na Waandishi wa habari na kwa Umaarufu wa Lil Wayne huena hata safari yenyewe ingekufa kutokana na kuzongwa kwa maswali pamoja na matukio ya picha. ambapo hata hivyo Amanda aliweza kupiga picha moja tu!.
LIL WAYNE ALISIMAMISHA NDEGE KWENDA KUSALIMIANA NA WANAJESHI.
Reviewed by Unknown
on
02:52
Rating:
No comments: