Recent Posts

IJUE BAGAMOYO KUPITIA TAMBO LANGU ELIMU KWAKO!!!.

TAMBO LANGU ELIMU KWAKO.
Tambo langu elimu kwako linahusu wilaya ya Bagamoyoni kuangalia jinsi ya jina la Bagamoyo lilivyokuja, pia wilaya hiyo ya Bagamoyo inayopatikana mkoani Pwani.
Bagamoyo ni mji mkubwa sana kihistoria kutokana na kuwepo na mambo mengi sana makumbusho ya kale na viongozi mbalimbali wa kikoloni waliokuwa wanapitia bagamoyo na kwenda  Zanzibar kwenye soko la Watumwa.
Kwanza nikianza na maana ya jina la Bagamoyo limetokana na hapo zamani watumwa walipokuwa wanasafirishwa kwenda Zanzibari kwenye soko kuuu la watumwa lazima wapitie mjini Bagamoyo, na wakifika mjini hapo hupumzika kwa ajili ya kusafirishwa, sasa kile kitendo cha kupumzika kwa amani, upendo na utulivu na pia huwa wanabwaga mioyo yao bila kuwa na mawazo ya aina yoyote ile ndio huitwa Bwaga moyo na sio Bagamoyo kama watu wanavyoita sasa hivi.
Kwa hiyo Bagamoyo limetokana na neno Bwagamoyo yaani ni kuubwaga moyo na ndio mpaka leo bado linaitwa bagamoyo.
Lakini pia bagamoyo kuna makumbusho ya aina mbalimbali  kama minyororo waliofungwa watumwa kipindi cha ukoni, kuna mawe, vikombe, nyumba, visima misikiti ambapo vitu hivi vyote vilitumiwa na wakoloni
Lakini pia bagamoyo kuna mbuyu mkubwa sana wa kikoloni unaosadikiwa kuwa na umri wa miaka mia ni karne moja, mbuyu huo ambapo inasemekana wamisionari na  wafanyabiara walikuwa wanakaa na kupumzika. hiyo ndio historia fupi ya kistoria kutoka mkoni pwani wilayani Bagamoyo.
 
IJUE BAGAMOYO KUPITIA TAMBO LANGU ELIMU KWAKO!!!. IJUE BAGAMOYO KUPITIA TAMBO LANGU ELIMU KWAKO!!!. Reviewed by Saidia Turuki on 07:40 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.