Lino International ambao ni waandaji wa shindano la Miss Tanzania 2014 wakishirikiana na Redds wamekutana leo jijini Dar es salaam na waandishi wa habari ili kuzungumza nao kuhusu skendo ya umri halisi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Baada ya skendo kukua juu ya Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu kuhusiana na umri wake baada ya kujitangaza kwa kusema anaumri wa miaka 18 wakati vitambulisho vikionyesha anamiaka 26 na picha mbali mbali kuzagaa katika mitandao ya kijamii hasa Instagram hali iliyozua utata kwa wapenzi wa Mashindano hayo ya walimbwende, ambapo kwa mujibu wa taarifa kamili ni kuwa Skendo hii haiwahusu mshindi wa pili Lilian Kamazima na watatu Jihhan Dimachk. ambapo mpaka sasaTaarifa zilizosamba kwenye mitandao ya kijamii Tanzania ni kwamba Sitti hakuwa mkweli na umri wake baada ya kusema anamiaka 18 huku vitambulisho vikionyesha anamiaka 26.
Kuhusu suala la passport na leseni zilizosambaa kwenye mitandao ya
jamii zikionesha amezaliwa mwaka 1989, Lundenga amesema wao huwa
hawangaali vitu hivyo wanachojali ni cheti cha kuzaliwa.
Na juu ya madai ya Rushwa Hashimu Lundenga amesema hakuna suala la yeye kupewa rushwa, ila Sitti Mtemvu ameshinda kihalali kwa kupitishwa na Majaji.
Kuhusu tuhuma za unene pia amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa.

UTATA JUU YA UMRI WA MISS TANZANIA 2014 SITTI MTEMVU, NA HATIMA KAMILI KUHUSU UMRI WAKE HALISI
Reviewed by Unknown
on
05:13
Rating:
No comments: