Msanii maarufu wa kundi la TMK Wanaume
Family YP Amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya Temeke
baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu.
Taarifa kwa mujibu wa Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family
Said Fella amesema kuwa ratiba ya mazishi bado haijapangwa ambapo kaka yake na
ndugu zake wanasubiriwa.
"ratiba ya mazishi bado haijapangwa, kaka yake na
ndugu zake wengine wanasubiriwa na mpaka mchana leo ndio tutajua
marehemu anazikwaje" alisema Fella.
Fella amesema marehemu alisumbuliwa na
kifua kwa muda sasa na alikuwa anatumia dawa,ambapo Alizidiwa siku chache
nyuma na kupelekwa hospitalini.
Fahamu kuwa Wazazi wake walifariki zamani ila
walezi wake wapo Keko na ndio msiba ulipo.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi Amen.
MSANII WA KUNDI LA TMK WANAUME FAMILY YESSAYA AMBIKILE [YP] AFARIKI DUNIA
Reviewed by Unknown
on
06:04
Rating:
No comments: