KUMBUKUMBU YA ABEID AMANI KARUME NI FUNZO KUBWA.
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kitaifa tangu kufariki kwa Raisi wa kwanza wa Zanzibar sheikh
Abeid Amani Karume miaka 43 iliyopita.
Raisi huyo wa kwanza wa Zanzibar aliuawa kwa kupigwa risasi huko visiwani Zanzibar, ambapo katika Uongozi wake Hayati Amani Abeid Karume, na Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere ambao wote,walitupatia Tanzania tunayoijua sasa hivi,ukiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Kiongozi huyo wa kwanza wa Zanzibar,kifo chake bado kimekuwa cha utata mpaka sasa,kwa kuwa
alivyouawa kiongozi huyo mpendwa wa Tanzania na Afrika,ambapo kwa ushirikiano na wanamapinduzi wengine visiwani,aliwezesha
kuung,oa utawala wa kisultani katika kipindi cha umwagaji damu.
Wapo walioamini kwamba Karume aliuawa na kikundi cha wauaji kwa lengo la kulipiza kisasi kutokana na chuki na uhasama wa kale,na wengine wakiamini kwamba kiongozi huyo aliuawa katika
jaribio la kijeshi lililoshindwa dhidi ya serikali yake.
Risasi nane zilitolewa mwilini kwake mwili wake ulipofikishwa kwenye Hospitali ya V. I. Lemin, mjini
Unguja kwa uchunguzi, sawa na idadi ya miaka minane ya utawala wake tangu 1964 hadi kifo
chake.
Ilikuwa hivi: Rais Karume na Makomredi wenzake
wa Chama cha Afro-Shirazi (ASP) alikuwa na mazoea ya kucheza karata, damma au dhumuna
kwenye ukumbi wa ofisi za makao makuu ya Chama hicho Kisiwandui, kila jioni kama sehemu ya mapumziko.
Siku hiyo alifika saa 11.00 jioni
akiwa na walinzi wake, akaingia ndani nao wakabaki nje kulinda.
Ikafika zamu yake kucheza; akawa anacheza na Mzee Maalim Shaha Kombo ambaye alionekana
kulemewa.
Ndipo Karume akamwita Mzee Mtoro Rehani ajitayarishe baada ya Kombo, naye akaitikia kwa kuaga kwanza aende msalani kujisaidia.
Sekunde chache baada ya hapo na kabla Mzee Mtoro Rehani hajarejea kutoka msalani, ghafla watu
wawili wenye silaha walivamia chumba alimokuwa Karume na wenzake na kumimina risasi
wakimlenga; na kufumba na kufumbua, akawa katika dimbwi la damu kimya, amepoteza uhai.
Hakuna mtu mwingine aliyeuawa mbali na kujeruhiwa tu, mmoja wao akiwa Katibu Mkuu wa
ASP, (sasa) Hayati Thabit Kombo Jecha.
Risasi uaji (the fatal bullet), mbali ya risasi zote, iliyochukua uhai wa Karume ilitoka kwenye bunduki
ya Luteni Hamoud Mohammed Hamoud wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT), ambaye ndiye
alikuwa kiongozi wa uvamizi huu na aliyefyatua risasi ya kwanza wakati Karume akicheza nawenzake.
Inasemekana, Hamoud aliuawa papo hapo na mlinzi wa Karume.
Wauaji wengine waliofuatana na Hamoud katika uvamizi huo ni Kapteni Ahmada Mohamed, Koplo
mmoja wa jeshi ambaye jina lake halijafahamika hadi leo, na raia mmoja aliyekwenda kwa jina la Ali
Khatibu Chwaya, ambao inaelezwa wote hao waliuawa kwenye mapambano ya silaha nje ya
eneo la tukio.
Dakika chache baada ya mauaji kutokea, alifika Kanali Ali Mahfoudhi na askari mwingine, Kapteni
Makame Hamis, wakauchukua mwili wa Karume na kuukimbiza hospitali.
Itakumbukwa, Kanali Mahfoudhi ni mmoja wa vijana wa Umma Party (UP) cha Abdulrahman Mohamed
Babu, kilichoungana na ASP baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 na kuunda Serikali ya mseto.
Ni kati ya vijana waliopelekwa Cuba kwa mafunzo ya kijeshi, na ni mmoja wa wapiganaji
walioendesha mapambano ya kisayansi usiku wa Mapinduzi na kukamata uwanja wa ndege mchana
Aprili, 1972.
Ni mmoja wa wanaharakati wa siasa za mrengo wa Kikomunisti ambao hawakutakiwa Zanzibar wakati wa utawala wa Karume, hivi kwamba kufuatia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26,
1964, Karume alishinikiza kwa Nyerere wapewe kazi Tanzania Bara aweze “kupumua” ambapo
Mahfoudhi alipewa cheo cha Mkurugenzi wa Operesheni katika JWT.
No comments: