LIVERPOOL YATUPWA NJE FA CUP YACHAPWA 2-1 NA ASTON VILLA.
>>Aston Villa imetinga fainali ya kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2000 baada ya
Fabian Delph kufunga bao la pili na la ushindi dhidi ya Liverpool katika mechi ya semi fainali.
Ushindi huo umeiacha Liverpool bila kitu msimu huu, Liverpool ilichukua uongozi kupitia Phillipe Coutinho ambaye alivamia lango la Aston Villa kabla ya kucheka na wavu licha ya kukabwa na wachezaji wa Villa.
Lakini Villa walisawazisha kupitia Christian Benteke aliyepata pasi kutoka kwa Delph.
Delph baadaye alifunga bao la pili baada ya kuwapita walinzi wa Liverpool na hivyobasi kutinga
fainali ya kombe hilo na Arsenal mnamo tarehe 30 ilioicharaza Reading 2-1 siku ya jumamosi.
SPORTS: LIVERPOOL YATUPWA NJE FA CUP YACHAPWA 2-1 NA ASTON VILLA.
Reviewed by Unknown
on
05:23
Rating:
No comments: