KENYA YAANZA KUWAWINDA AL-SHABAAB.
Kupitia BBC imeripotiwa kuwa Ndege za kijeshi za Kenya zime shambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Al-shabaab katika taifa
jirani la Somalia.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kuwa Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, ambapo maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao
kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Sambamba na hayo imedaiwa kuwa Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawaja fanya hivyo.
#Fahamu: Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kufanya dhidi Al-shabaab ambao wiki iliyopita walifanya mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa Nchini humo.
Aidha Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Hata hivyo Msemaji wa jeshi la Kenya ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani
siku ya jumapili usiku katika eneo hilo, licha ya kuwa hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo
yaliotolewa.
No comments: