Recent Posts

NEWS: ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIFUNGULIA NYUMBANI.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIFUNGULIA NYUMBANI.

>>MKAZI mmoja wa eneo la Mkwajuni katika Kijiji cha Malagarasi, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, Pendo Madumu, amenusurika kifo kufuatia kuvuja
damu nyingi baada ya kujifungulia nyumbani kwa njia za kienyeji.

Akizungumzia tukio hilo hapo jana, ndugu wa mwanamke huyo ajulikanae kwa jina la Justina
Marko, alisema kuwa ndugu yake alitokwa na damu nyingi muda mfupi baada ya kujifungua na
kuzidiwa hali iliyowalazimu kukodi pikipiki na kumkimbiza katika kituo cha afya cha Nguruka.

“Alianza kupatwa na uchungu mida ya saa kumi na moja, ilipofika saa kumi na mbili akajifungua,
alijifungua salama na akaoga sambamba na kunywa uji baada ya muda akaanza kutokwa damu
na muda ulivyozidi nguvu zote zilikuwa zikimwishia mpaka tukaanza kumwagia maji ndipo
tukaona tumwahishe kwenye hospitali,”alisema
Justina.

KAY-STALLION TZ ilishuhudia mwanamke huyo akiwa amechubuka vidole vyake vya miguu kutokana na kuburuza miguu yake chini wakati jitihada za
kumfikisha kituo cha afya zikifanywa na ndugu zake.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Nguruka, Dr Stanford Chamgeni, ameeleza kuwa
mwanamke huyo walimpokea kituoni hapo hali yake ikiwa mahtuti baada ya kujifungulia nyumbani.

Alisema kuwa, baada ya kujifungua kule kijijini yeye na mtoto walikuwa wazima na vitu vyote vilivyokuwa tumboni vilitoka vyote kwa usalama,
lakini tatizo la kutoka damu ndio lilimfanya kupoteza fahamu na kufikishwa kituoni akiwa
mahututi.

“Baada ya kufikishwa tulianza kumpa maji yanayohusika mikono yote miwili, tukampa na dawa nyingine na hivi sasa anaongezewa damu, ila alipoanza kupata maji tu ya kutosha akapata fahamu, lakini kama angekosa usafiri akakaa
masaa mawili zaidi kwa kweli mama huyu alikuwa apoteze maisha” alisema Chamgeni.

Hata hivyo Dr Chamgeni alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha kwamba wanawahi kwenye vituo vya
afya wakati wa kujifungua ili kuepuka vifo visivyo vya lazima kwani ni si salama kujifungulia
nyumbani.

“Sasa hivi kituo chetu kinajitahidi kutoa matibabu sahihi kwa wajawazito ili kuhakikisha wanajifungua salama, kwa hiyo ni vizuri wawahi kuja kujifungua
kituo cha afya” alisisitiza

NEWS: ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIFUNGULIA NYUMBANI. NEWS: ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIFUNGULIA NYUMBANI. Reviewed by Unknown on 19:08 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.