Recent Posts

NEWS: SHIBUDA HANA MPANGO NA ACT-TANZANIA.

SHIBUDA HANA MPANGO NA ACT-TANZANIA.

Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), John Shibuda amekataa kuhusishwa na Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), akisema hana mpango wa kujiunga
nacho.

Shibuda ambaye ameshatangaza kutogombea ubunge kupitia CHADEMA katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu, "sitagombea kupitia CHADEMA lakini nisilishwe
maneno…siendi kwenye chama hicho cha ACT.”

Kauli ya Shibuda imeondoa uvumi ulioenea kwamba angejiunga na ACT baada ya kuwa kwenye
mgogoro kwa muda mrefu na CHADEMA.

Akichangia hoja ya muswada wa sheria ya makosa ya mtandao bungeni wiki iliyopita, Shibuda
alitumia dakika mbili kuweka sawa uvumi huo na kusema, “sitaki kusemewa…nitasema mwenyewe
kuhusu mstakabali wangu kisiasa. Huu ni uzandiki.”

Hii si mara ya kwanza kwa Shibuda kuhusishwa na mpango wa kuhamia katika vyama vingine vya upinzani.

Mwishoni mwa mwaka jana pia kulikuwa na uvumi kwamba yuko kwenye mazungumzo ya kukinunua Chama cha TADEA kinachoongozwa na Lifa Chipaka.

Hata hivyo, Shibuda alikanusha uvumi huo akisema analishwa maneno.......

Sambamba na hayo KAY-STALLION TZ iko kwenye maandalizi ya kukuletea wewe msomaji wa habari zetu makala maalum ambazo kila wiki tutakuwa tukijaribu kuangalia mustakabali wa taifa la Tanzania
kuelekea uchaguzi mkuu unao tarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi wa kumi hapa tutaangalia na
kuchambua mambo mbalimbali ya kisiasa na kuona ni jinsi gani wanasiasa wanavyojiweka
katika kipindi hiki cha mwaka wa uchaguzi sambamba na maoni mbalimbli ya wananchi......
USIKOSE NI KUANZIA WIKI IJAYO.

NEWS: SHIBUDA HANA MPANGO NA ACT-TANZANIA. NEWS: SHIBUDA HANA MPANGO NA ACT-TANZANIA. Reviewed by Unknown on 04:37 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.