KENYA YATAMBUA MOJA YA WAUAJI WA GARISSA.
Serikali ya Kenya imemtambua mmoja wa wapiganaji waliohusika katika mauaji ya chuo kikuu
cha Garissa, yaliyo tokea wiki iliyo pita Nchini humo kuwa ni mtoto wa afisa wa serikali.
Msemaji wa wizara ya ndani, alisema kuwa Abdirahim Abdullahi ni miongoni mwa watu 4 walio shambulia chuo kikuu cha Garissa siku ya Alhamisi wiki iliyopita na kuwaua watu 148.
Abdirahim Abdullahi alitambulika kuwa ni mtoto wa kiume wa Chifu wa eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya na alidaiwa kutoweka na baada ya tukio ambapo anahofiwa kuwa yupo nchini Somalia.
Hata hivyo washukiwa wengine katika shambulio hilo takribani 5 walikamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo ambayo ni mabaya zaidi kuwahi kutokea na wapiganaji wa kundi la Al-shabaab.
No comments: