TIMU YA FENERBAHCE YA SHAMBULIWA NA MAGAIDI.
>>Basi la kilabu ya Fenerbahce lilifyatuliwa risasi na magaidi baada ya kilabu hiyo ya Uturuki kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi kilabu ya Rizespor.
Dereva wa basi hilo alipelekwa hospitalini lakini hakuna mchezaji aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hilo ambalo lilitokea wakati walipokuwa wakielekea katika uwanja wa ndege wa Trabzon.
Waziri mkuu wa taifa hilo Ahmet Davutoglu amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
Basi la kilabu ya fenerbahce nchini Uturuki Shrikisho la soka nchini Uturuki lilishtumu shambulio hilo huku katibu mkuu wa kilabu hiyo
Mahmut Uslu akisema kuwa kitendo hicho ni cha makosa.
''Tulikuja hapa kucheza soka'' alisema Uslu ambaye alikuwa katika basi hilo wakati wa shambulio hilo.
SPORTS: TIMU YA FENERBAHCE YA SHAMBULIWA NA MAGAIDI.
Reviewed by Unknown
on
04:22
Rating:
No comments: