Recent Posts

ULIIPATA HII: MZEE MWENYE WAKE 39, WATOTO 94, WAJUKUU 33!!.

ULIIPATA HII: MZEE MWENYE WAKE 39, WATOTO 94, WAJUKUU 33!!.

Wakati Nchi nyingi katika bara la Asia zikijitahidi kupunguza ongezeko la watu kwa kutengeneza mfumo wa uzazi wa mpango lakini kumbe kuna watu hawa hafikiani na jambo hilo.

Mzee mmoja kutoka Nchini India, Ziona Chana amejipatia umaarufu duniani baada ya kupiga picha na familia  yake yenye  wake 39, Watoto 94, na Wajukuu 33 huku shirika la habari la Reuters la Nchini humo lilifanya mazungumzo naye kuhusu ukubwa wa familia aliyo nayo na kudai hatojali iwapo atapata wake
wengine wa kuwaoa.

Ziona Chana, anaishi katika kijiji kimoja cha mbali, kaskazini mashariki mwa India, wote yeye pamoja na wake, watoto, na wajukuu wanaishi katika nyumba moja yenye vyumba 100, katika kijiji cha milimani kwenye jimbo la Mizoram, karibu na mpaka na Myanmar na Bangladesh.

"Kuna wakati nilioa wake kumi katika kipindi cha
mwaka mmoja na Wake zangu wanaishi pamoja katika bweni moja
kubwa karibu na chumba changu na huwa ninapo pata muda wa kupumzika huwa na  pendelea kuwa na wake saba au nane kila wakati" alisema Ziona.

ULIIPATA HII: MZEE MWENYE WAKE 39, WATOTO 94, WAJUKUU 33!!. ULIIPATA HII: MZEE MWENYE WAKE 39, WATOTO 94, WAJUKUU 33!!.
Reviewed by Unknown on 03:25 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.