ENTERTAINMENT NEWS: KAMA JUSTIN BIEBER ASIPO ZINGATIA ONYO LA BIG SEAN KUJIWEKA MBALI NA MPENZI WAKE HUENDA LIKAZALIWA BEEF MATATA.
KAMA JUSTIN BIEBER ASIPO ZINGATIA ONYO LA BIG SEAN KUJIWEKA MBALI NA MPENZI WAKE HUENDA LIKAZALIWA BEEF MATATA.
Kitendo cha star wa Pop Nchini Marekani Justin Bieber kumbambia mpenzi wa Rapa Big Sean, Ariana Grande katika show yake mjini L.A, kimetokea kuwa chukizo kwa Big Sean na kumfanya kuapa kumfundisha adabu asipo zingatia kujiweka mbali na mpenzi wake huyo.
Licha ya mastaa hao kuwa na ukaribu wa kirafiki zaidi pia kufuatia kutengeneza Hot leading record ya 2012 ya "As long as you love me" Big sean ali Tweet ujumbe katika acount yake ya Twitter kumtaka Justin asijihusishe na kitendo kama hicho cha kumbambia mpenzi wake ambacho alikifanya katika show ya ziara yake Ariana Grande ya "HONEYMOON TOUR" huko Los Angels, Marekani jumatano wiki hii.
Katika show hiyo, Ariana Grande ali perform nyimbo mbili pamoja Justin Bieber ikiwemo 'As Long As You Love Me' na 'Love me harder'.
Big Sean kupitia Twitter aliandika ujumbe kumuhusu J.Bieber unasomeka hivi “ This kid is
about to learn not to touch my girl like that. Beliebe that. ”
Ukiwa na maana kuwa "Huyu mtoto atajifunza kutomschika msichana wangu kama hivyo" akimalizia na neno 'Beliebe that' kuashilia 'Amini hilo'.
No comments: