NEWS: MABASI MAWILI: KAMPUNI YA RATCO NA NGOLIKA PAMOJA NA GARI DOGO YA GONGANA NA KUUWA WATU 10 NA KUJERUHI 35 TANGA.
MABASI MAWILI: KAMPUNI YA RATCO NA NGOLIKA PAMOJA NA GARI DOGO YA GONGANA NA KUUWA WATU 10 NA KUJERUHI 35 TANGA.
Watu 10 wamefariki dunia papo hapo na wengine 35 kujeruhiwa vibaya siku ya Jana ,baada ya mabasi 2 ya abiria
na gari dogo kugongana.
Katika ajali hiyo majeruhi 7 hali zao zilikuwa mbaya,ambapo walikimbizwa Hospitali ya wilaya ya Handeni katika kituo cha afya cha mkata mkoani Tanga kwa ajili ya matibabu zaidi.
Ajali hiyo ilitokea jana mchana katika kijiji cha Mbweni kilichopo mkata,wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Juma Ndaki,alizungumza kwa njia ya simu na KAY-STALLION TZ, na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aliyekuwa akitaka
kulipita kasi basi bila kuchua tahadhari zozote.
Kamanda huyo aliyataja mabasi hayo kuwa ni basi la kampuni ya RATCO lenye namba za usajili T665 CBR, basi la kampuni ya NGORIKA lenye namba za usajili T770 BKW,na gari dogo aina ya PASSO lenye namba za usajili T628 CXE.
Katika ajali hiyo dereva wa gari dogo alikuwa anatokea Morogoro kwenda Arusha na alipofika eneo la Mbweni akawa anataka kulipita basi la
Ngorika,ndipo alipoanza kulipita akakutana na basi na abiria saba walikufa papo hapo pamoja na
dereva wa gari dogo wote walipoteza maisha.
Katika basi la RATCO kamanda alisema kuwa dereva alivunjika mguu wa kulia na abiria wote walinusurika kifo,lakini walipata majeraha madomadogo.
Kaimu huyo alimalizia kwa kusema kuwa ajali hiyo ya magari matatu kugongana ilisababishwa na
mwendo kasi wa madereva.
No comments: