GOODLUCK JONATHAN APATA UPINZANI MKALI
URAISI NIGERIA.
Nusu ya matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini Nigeria yakiwa yame tangazwa baadhi ya sehemu, mgombea kutoka chama kikuu cha
upinzani Muhammadu Bahari anaongoza dhidi ya raisi aliye madarakani Goodluck Jonathan.
Hata hivyo majimbo ya kusini yenye idadi kubwa ya watu kama vile Lagos na Rivers bado hayaja tangaza matokeo na mwandishi wa BBC, mjini Abuja alisema mchuano ni mkali.
Tume ya uchaguzi Nchini humo ilisema kuwa itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi hii leo jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadae ili kumjua mshindi wa uraisi nani nchini humo.
NEWS: GOODLUCK JONATHAN APATA UPINZANI MKALI
URAISI NIGERIA.
Reviewed by Unknown
on
04:12
Rating:
No comments: