ASKOFU GWAJIMA: SIWEZI KUCHAGULIWA MARAFIKI.
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima,Josephat Gwajima jana alihubiri huku akiwa katika kiti cha
magurudumu matatu,ambacho kiti hicho mara nyingi hutumiwa na walemavu wa miguu,na kusema kuwa hawezi kuwatupa marafiki zake wa muda mrefu, ambao ni pamoja na mbunge wa monduli (ccm) Edward Lowassa na katibu mkuu wa chadema Dk Willbrod Slaa kwa kuwa ni marafiki zake wa siku nyingi.
Askofu huyo pia aliwataka waumini wote wa kanisa hilo kufika katika kituo cha polisi,Alhamisi ya wiki hii siku ambayo atakwenda kukamilisha mahujiano dhidi ya tuhuma za kumtukana Askofu mkuu wa kanisa jimbo kuu la Dar es salaam Polycarp Kardinali Pengo.
Akihubiria mamia ya waumini waliofika kanisani hapo,kwa ajili ya ibada ya pasaka hapo jana,Gwajima alisema kumekuwa na uvumi
kwamba kuhojiwa kwake na polisi kulitokana na kuwakaribisha wanasiasa hao kanisani kwake kwa
nyakati tofauti.
Alicho dai yeye ni kuwa ali fahamiana na Lowassa tangu mwaka 1996 wakati huo mbunge alikuwa waziri wa Ardhi na tangu kipindi hicho amekuwa mtu wake wa karibu sana.
Alifafanua kuwa pia alifahamiana na Dk Slaa mwaka 1994, kabla hajagombea nafasi ya uraisi
kupitia chadema na kwamba tangu wakati huo amekuwa rafiki wa familia moja.
Alimalizia kwamba hawezi kuchaguliwa marafiki, "Slaa na Lowasa ni watu wangu wa karibu
hata kabla hawajawa na ndoto za kugombea uraisi", alisema Gwajima
No comments: